Tuesday, October 4, 2011

CHADEMA:TUTAIFIKISHA CCM MAHAKAMANI

CHASEMA SHERIA, MAADILI,TARATIBU VILIKIUKWA, MUKAMA WA CCM ALIA NA WASIMAMIZINeville Meena, Igunga
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza kwamba kitapinga mahakamani, matokeo ya ubunge wa Jimbo la Igunga ambayo yalimpa ushindi mgombea wa CCM, Dk Dalaly Kafumu.Katika taarifa yake kuhusu uchaguzi huo aliyoitoa jana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alidai kwamba kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa sheria, taratibu na maadili katika uendeshaji wake.

Hata hivyo, Mbowe alisema licha ya kupoteza jimbo hilo, chama chake kinajivunia mafanikio makubwa kilichopata katika muda mfupi kwa kupata kura nyingi ikilinganishwa na CUF ambacho licha ya kuwa na mtaji wa kura 11,000 kilizopata katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, kiliambulia kura 2,014.

Dk Kafumu alishinda kwa kupata kura 26,484 kati ya kura 52,487 halali zilizopigwa, sawa na asilimia 50.4, akiwashinda wenzake saba wa vyama vingine.

Mgombea wa Chadema, Joseph Kashindye wa Chadema alipata kura 23,260 sawa na asilimia 44.3 akifuatiwa na Leopold Mahona aliyepata kura 2,104 sawa na asilimia nne.

Akizungumzia nia yake ya kwenda mahakamani, Mbowe alisema CCM kilitumia kiasi kikubwa cha fedha na rasilimali nyingine katika uchaguzi huo kuliko ambavyo imewahi kutokea katika chaguzi nyingine ndogo na kwamba kulikuwa na hujuma za wazi zilizofanywa, hivyo kukiukwa sheria na maadili yanayoongoza uchaguzi.

Alisema kulikuwa na vitendo vya rushwa vilivyofanywa na chama kimoja cha siasa na kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), ilishindwa kuchukua hatua licha ya kuwa na uwezo wa kufanya hivyo kisheria.

Mwenyekiti huyo wa Chadema pia aliilaumu polisi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) akidai kwamba wamechangia kuharibu mchakato mzima wa uchaguzi huo mdogo.

Alidai kwamba CCM kilitumia chakula cha msaada kwa waathirika wa njaa kama silaha ya kisiasa kwenye uchaguzi na kwamba wananchi wa Igunga walipewa mahindi wakirubuniwa ili wakipigie kura chama hicho.

Viongozi wa Serikali
Mbowe alisema ushindi wa CCM pia ulichangiwa na chama hicho kupuuza sheria za uchaguzi kwa kutumia viongozi na rasilimali za umma kwa ajili ya kukinufaisha.

“Mawaziri na viongozi kadhaa waandamizi wa Serikali walifanya kampeni za waziwazi kwa niaba ya CCM na kwa kutumia magari na muda wa Serikali… viongozi haohao wa Serikali walitumia rasilimali za Serikali kama chakula cha msaada, ahadi ya kiserikali kuhusu mgawo wa fedha za ujenzi wa daraja na ahadi ya kutoa pembejeo kwa wakulima,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo ya Mbowe.

Kuhusu NEC, alisema kulikuwa na ukiukwaji wa Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 kutokana na Tume hiyo kuwanyima haki ya kupiga kura baadhi ya watu ambao utambulisho wao ulikuwa na utata.

“Mpigakura yeyote ambaye utambulisho wake ni wa mashaka, anatakiwa aruhusiwe kupiga kura baada ya kupewa onyo na kujaza tamko la kisheria kuthibitisha kuwa ana haki ya kupiga kura katika kituo husika,” alisema Mbowe na kuongeza:

“Licha ya msimamo huo wa kisheria, NEC ilitoa maelekezo kwa maandishi kwa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura yanayokataza wapigakura wasiokuwa na kadi za kupiga kura, kutoruhusiwa kupiga kura.”

Alisema mbali na kukiuka Sheria ya Uchaguzi, maelekezo hayo yalitoa mwanya wa ununuzi wa kadi uliofanywa na chama cha siasa kimojawapo na kwamba ndiyo chanzo cha watu wachache kujitokeza kushiriki uchaguzi huo, ikilinganishwa na idadi ya walioandikishwa.

Wapigakura walioandikishwa katika Jimbo la Igunga ni 171,019 na waliojitokeza kupiga kura mwaka huu ni 53,672 sawa na asilimia 31.3, kukiwepo ongezeko la asilimia 2.7 ikilinganishwa na idadi ya waliopiga kura mwaka jana ambao walikuwa 49,013 sawa na asilimia 28.6 ya 171,077 waliokuwa wamejiandikisha.

Mbowe alisema kutokana na upotoshwaji wa kisheria uliofanywa na NEC, ipo hatari ya siku za usoni kukatokea madhara makubwa zaidi kwa watu walioandikishwa katika Daftari ya Kudumu la Wapigakura kunyimwa haki yao.
“Kwa rekodi yake hii na kwa sheria za uchaguzi zilizopo, NEC haina tena sifa ya kuweza kusimamia kazi hii muhimu ya kusimamia kura ya maoni itakayopitisha Katiba mpya ya Tanzania. Chadema itafanya kosa kubwa kama itafumbia macho ukweli huu,” alisema Mbowe.

Uchaguzi wa Igunga pia uliwashirikisha wagombea wengine ambao ni Steven Mahuyi (AFP) aliyepata kura 235, Hassan Rutegama (Chausta) aliyepata kura 182, Said Cheni DP kura 76 na Hemed Ramadhani (SAU) kura 63.

CCM walaumu wasimamizi

Kwa upande wake, CCM kimetoa shutuma kali kwa wasimamizi wa uchaguzi vituoni, kikisema kwamba walisababisha kupungua kwa kura zake katika uchaguzi huo.

Juzi, baada ya Dk Kafumu kutangazwa mshindi, Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama alidai kuwa chama chake kingeweza kupata ushindi mkubwa zaidi lakini kilihujumiwa na wasimamizi ambao alidai kuwa wengi walikuwa na mapenzi kwa Chadema.

“Ushindi huu unaonyesha kwamba kuna uongozi mpya ndani ya nyumba. Tumefanya vizuri lakini kama si hujuma za wasimamizi tungeshinda kwa kishindo kikubwa zaidi,” alisema Mukama.

Tuhuma hizo za Mukama kwa wasimamizi zinatokana na matokeo ambayo yanaonyesha kuwa licha yaa kushinda, CCM kimefanya vibaya katika jimbo hilo ikilinganishwa na uchaguzi wa mwaka jana wakati mgombea wake, Rostam alipopata ushindi wa kura 35,674 sawa na asilimia 72.7 ya kura halali zilizopigwa akimshinda aliyekuwa mgombea wa CUF, Mahona ambaye alipata kura 11,321 sawa na asilimia 23.1.

Kauli ya Mukama haikuwa ya kwanza kutolewa na viongozi wa CCM dhidi ya wasimamizi kwani siku ya uchaguzi, Oktoba 2, mwaka huu, Katibu wa Siasa na Mambo ya Nje wa chama hicho January Makamba alitoa tuhuma kama hizo akidai kwamba baadhi ya wasimamizi walikuwa wakiwapa wapigakura karatasi za kupigia kura ambazo tayari zilikuwa na alama ya tiki kwa mgombea wa Chadema.

Hata hivyo, Msimamizi wa Uchaguzi Igunga, Protase Magayane alipuuza tuhuma hizo akisema kuwa kulikuwa na fursa kwa vyama na umma kwa ujumla kutoa pingamizi pale wa wasimamizi hao walipoteuliwa kwa mara ya kwanza.

Alisema vyama vya siasa vilipaswa kufanya mapitio ya makini katika orodha ya wasimamizi na kwamba hatua zingechukuliwa kabla ya uchaguzi, badala ya kusubiri kulalamika siku ya uchaguzi.

CCM yairushia kombora Chadema
CCM kimeibuka na kudai kuwa vurugu za wanachama wa Chadema ndicho chanzo cha idadi kubwa ya watu kutojitokeza kupiga kura.

Katika uchaguzi huo, idadi kubwa ya watu hawakujitokeza kupigakura kwani kati ya watu 171,019 waliojiandikisha ni 53,672 tu sawa na asilimia 31.3 waliojitokeza Jumapili iliyopita.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema mabadiliko makubwa ya uongozi ndani ya chama hicho ndiyo yaliyokipa ushindi Igunga.

“Ushindi huu ni uthibitisho kuwa mapinduzi makubwa yaliyofanyika ndani ya chama yamezaa matunda na yanaungwa mkono na wananchi na ndiyo maana tumeibuka washindi Igunga,” alisema Nnauye na kuongeza:

“Kutokana na fujo za Chadema, idadi kubwa ya watu haikujitokeza kupiga kura. Uchaguzi huu umeonyesha jinsi Chadema walivyokuwa wabakaji wa demokrasia. Watanzania wanatakiwa kuikataa hali hii, hakuna demokrasia ya namna hii.”

Nnauye alisema kitendo cha CCM kushinda udiwani katika Kata 17 kati ya 22 katika Mikoa ya Arusha, Dodoma, Iringa, Manyara, Mara, Mbeya, Mwanza, Rukwa, Ruvuma na Sinyanga ni ishara kuwa hicho kinakubalika.

Mapokezi mazito
Nnauye alisema viongozi wakuu wa CCM ambao walikuwa Igunga watafanyiwa mapokezi mazito Jumamosi ijayo, Dar es Salaam.

“Kesho (leo) watapokewa na wananchi mkoani Singida, Oktoba 6, watakuwa Dodoma, Oktoba 7 watakuwa Mkoa wa Pwani na Oktoba 8 watakuwa Dar es Salaam. Tumefanya hivi kwa lengo la kuwashukuru wananchi,” alisema

Tuesday, September 27, 2011

Helikopta ya Chadema yatikisa Igunga

MBILI ZA CCM ZASHINDWA KUTUA ZABAKI KIA, YA  CUF KUPASUA ANGA LEO 
Waandishi Wetu, Igunga
WAKATI Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kilitikisa anga la Igunga baada ya kuanza kutumia helikopta kufanya kampeni zake, zile mbili za wapinzani wao, CCM zikishindwa kuwasili jimboni humo na kubaki Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kutokana na sababu za kiufundi.Wakati Chadema ikipasua anga na mbili za CCM zikibaki KIA, helikopta ya Chama cha Wananchi (CUF) nayo imeshindwa kutua Igunga jana na sasa inatarajiwa hapa leo.

Helikopta ya Chadema ilianza kuonekana katika anga la Igunga saa 10:40 jioni ikiwa na maandishi makubwa ya chama hicho na rangi ya bluu.Ujio wa helikopta hiyo ulivuta kwa muda idadi kubwa ya wananchi waliokuwa kwenye Viwanja vya Sabasaba wakisubiri ujio wa helikopta mbili za CCM, ambazo awali, ilielezwa kuwa zingewasili saa 8:00 mchana.

Baadaye ilielezwa kwamba helikopta hizo za CCM zingetua Igunga saa 11:30 jioni zikiwa na makada wa chama hicho akiwamo Katibu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Bumbuli, January Makamba.

Hata hivyo, ilipofika saa 12:00 jioni, Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde akitumia gari la matangazo la Bendi ya muziki ya ToT Plus alitangaza kwamba helikopta hizo zisingeweza kutua Igunga kutokana na sababu za kiufundi.
Alisema zilichelewa kupata vibali kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam na kwamba baada ya kutua KIA ilishauriwa kuwa ni vyema zilale hapo.

Alisema kama helikopta hizo zingeondoka KIA jana jioni na kufika hapa usiku wakati tayari kungekuwa na giza kitu ambacho kisingekuwa kizuri kiusalama. Alisema helikopta hizo sasa zitawasili leo saa 4:00 asubuhi.

Matumizi hayo ya helikopta yanawafanya wananchi wa Igunga kushuhudia kampeni nzito na za aina yake tangu kufanyika kwa uchaguzi wa kwanza wa vyama hivyo mwaka 1994 na Rostam Aziz kushinda.Jimbo hilo lenye wapiga kura 170,000 katika vijiji 96, halijawahi kushuhudia kampeni nzito kiasi hicho zinazohanikizwa na magari yenye vifaa vya kisasa vya muziki.

Habari kutoka ndani ya CCM, zinaeleza kuwa katika kujihakikishia kura katika kipindi hiki cha lala salama, chama hicho kitawatumia makada wake, Makamba na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli wanaoelezwa kuwa na ushawishi mkubwa.

Kulingana na vyanzo mbalimbali vya habari, Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa aliyekuwa mgeni rasmi katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za CCM anatarajiwa kurudi tena hapa keshokutwa.Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe naye aliwasili hapa jana kuongeza nguvu kwa viongozi wa chama hicho ambacho idadi kubwa ya wabunge wake wameweka kambi hapa.

Helikopta ya CUF
Kwa upande wake, CUF kinatarajiwa kuanza kutumia helikopta yake kuanzia leo huku Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Juma Duni Haji akitarajiwa kufunga pazia la kampeni za chama hicho ambazo, awali zilitarajiwa kufungwa na Katibu Mkuu wake ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad.

Akizungumzia na waandishi wa habari jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius Mtatiro alisema kampeni hizo sasa zitafungwa na Haji anayetarajia kuwasili wakati wowote katika kipindi hiki cha mwisho wa kampeni.Mtatiro alisema tayari wabunge wa chama hicho  akiwamo Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Zanzibar) Ismail Jussa wanaendelea na kampeni jimboni humo.

CCM, Chadema vyatuhumiana
Kiwewe cha uchaguzi huo kimezidi kutesa vyama vya CCM na Chadema, baada ya kuendelea kutuhumiana huku chama tawala kikidai kunasa kile ilichokiita mpango wa siri wa wapinzani wake hao wa kujitangazia ushindi kabla Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kufanya hivyo.

Chadema nacho kimekituhumu CCM kwamba kimeandaa mpango wa kupeleka wapigakura mamluki kutoka katika baadhi ya mikoa ukiwamo Dar es Salaam.

Jana, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Steven Wassira aliwaambia waandishi wa habari mjini hapa kwamba Chadema kimepanga mpango huo wenye lengo la kuwaandaa wanachama wake waone wameibiwa kura pindi CCM kitakapotangazwa mshindi.“Tunazo taarifa za uhakika kuwa wamepanga kutumia magari ya matangazo kutangaza kuwa Chadema imeshinda, hata kabla ya kura kuhesabiwa ili wapate leseni ya kuanzisha vurugu,” alisema Wassira.

Wassira ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano), alisema tayari CCM wameviarifu vyombo vya ulinzi na usalama ili kuchukua hatua na pia kuwaelimisha na kuwasihi wananchi kutoingia katika mtego huo.

“Lengo ni kuwaharibu vijana kisaikolojia kwamba yakitangazwa matokeo tofauti waone wamechakachuliwa kura zao na CCM. Tunawasihi Chadema na wanachama wao watulie wakati wananyolewa,” alisema Wassira.

Wassira alisema wanakusudia kutumia mikutano ya hadhara ya kampeni iliyobakia wiki hii ya lala salama, kuwaeleza wananchi juu ya mpango huo wa Chadema ambao alidai hauwatakii mema wananchi wa Igunga.

Hata hivyo, Mratibu wa Kampeni za Chadema  Igunga, Mwita Waitara alikanusha vikali madai hayo akisema hawana sababu ya kufanya hivyo kwa kuwa wananchi wameshafanya uamuzi wa kuikataa CCM.“Wassira anafahamu utaratibu wa kutangaza matokeo ulivyo kwamba Chadema hatuna uwezo huo. Hivi kama tulikuwa na uwezo huo kulikuwa na sababu gani ya kufanya kampeni na kuteua hadi mawakala?,” alihoji.

Alikishutumu CCM akidai kuwa kina mpango wa kuingiza watu 1,050 kutoka Mikoa ya Dar es Salaam, Singida na Shinyanga ili watumie shahada bandia kukipigia kura chama hicho tawala.Waitara alidai kuwa watu 500 watatoka Dar es Salaam, 300 Singida na 250 Shinyanga lakini akasisitiza kuwa Chadema kina mtandao mpana na kitahakikisha kinazuia mpango huo usifanikiwe.

Chagonja atua Igunga

Kamishina wa Polisi anayeshughulikia Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja jana aliwasili hapa na kusema polisi watakabiliana na yeyote atakayejaribu kuanzisha vurugu.“Nasema vurugu sasa basi na ninaonya yeyote atakayejaribu kutuchokoza tutakabiliana naye kwa nguvu zote… wananchi waende kwa uhuru vituoni kupiga kura,” alisema.

Kwa upande wake, Naibu Kamishina wa Polisi anayeratibu usalama Igunga, Isaya Mngulu amesema polisi wamefungua vituo tisa kwa ajili ya kukabiliana na matukio ya vurugu yatakayojitokeza.

Alisema vituo hivyo vina vifaa vyote vya kisasa yakiwamo mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha na kwamba vikosi vimejizatiti kukabiliana na hali yoyote ya vurugu itakayojitokeza.

Alivitaja vituo hivyo kuwa vipo katika maeneo ya Simbo, Mwisi, Nkinga, Sungwisi, Ziba, Mwanshimba na Itumba na kwamba kila kituo kina polisi wa kutosha wenye uzoefu wa kukabiliana na kila aina ya vurugu.

Katika kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unafanyika kwa amani na usalama, askari mgambo 325, Magereza wanane na polisi 94 watatumika katika kusimamia zoezi la upigaji kura katika vituo vyote 427.

Maandalizi yakamilika
Msimamizi wa Uchaguzi Igunga, Protas Magayane alisema jana kwamba vifaa vyote kwa ajili ya upigaji kura vipo tayari na vitaanza kusambazwa katika vituo vyote Jumamosi.

Magayane alisema orodha ya wapiga kura itabandikwa vituo kesho Alhamisi na kuwataka wale wote waliojiandikisha waende kuhakikisha majina yao na kufahamu vituo watakavyotumia kupiga kura.

Alisema wasimamizi wa vituo vya uchaguzi wapatao 427 waliapishwa jana na kwamba NEC itafanya kikao na viongozi wa vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi huo ili kuwekana sawa.

CUF nayo yapata homa
CUF nacho kimetoa shutuma mbalimbali dhidi ya CCM ikiwamo ya kuingiza makontena ya sukari wilayani Igunga kwa lengo la kugawa kwa wananchi kama njia ya kurubuni wananchi wakipigie kura.

Tuhuma nyingine za CUF kwa CCM ni kuwa  kinatarajia kuingiza kundi la makomandoo waliomaliza mafunzo na semina katika Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kuwatisha wapiga kura siku za mwisho za kampeni na uchaguzi.

Tuhuma hizo zilitolewa jana Mtatiro alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa.

Alisema tayari chama hicho kimepata taarifa za kuaminika kuwa kuna makontena yanayotarajia kusafirishwa kutoka Mara kwenda Igunga kwa ajili ya kugawanywa kwa wapiga kura. Bila kutaja kiasi alisema zinatarajiwa kuingia Septemba 29.

“Hii ni rushwa, haiwezekani kipindi hiki cha uchaguzi Serikali ya CCM kuleta kontena za sukari... tunataka Igunga ipate mbunge halali atakayechaguliwa na wananchi na sisi tumejipanga kuzuia jaribio hilo,” alisema Mtatiro.

Pia alidai kwamba chama hicho kimepanga kugawa chakula cha msaada nyumba kwa nyumba siku moja kabla ya kupiga kura na kwamba mpango huo umekamilika na magari yameandaliwa kufanya kazi hiyo Septemba 31 na Oktoba Mosi.

Akijibu tuhuma hizo Mratibu wa Kampeni wa CCM, Mwigulu Nchemba alikanusha na kusema wapinzani wao hao wana maralia ya uchaguzi.

Nchemba alisema kambi inayodaiwa ilifanyika siku nyingi na shughuli zake ziliisha... “Kambi tulishamaliza na sasa hakuna kinachoendelea, CCM hatuna mpango wa kuingiza vijana katika mji huu kutoka nje kwa ajili ya uchaguzi.”

Kuhusu chakula alisema Serikali imekuwa ikigawa chakula cha msaada katika maeneo mbalimbali yenye njaa na ilianza kufanya kazi hiyo kabla ya uchaguzi.

“Wanasema tunataka kugawa chakula Septemba 31 na Oktoba Mosi hapa Igunga? Siyo kweli kama tunafanya hivyo kwa ajili ya uchaguzi. Serikali inagawa chakula cha msaada katika maeneo yote ya njaa ikiwamo Igunga” alisema Nchemba.
SOURCE:mwananchi

USHABIKI,UPENZI NA IMANI KWA CHAMA

MAMBO YA IGUNGA

Monday, September 26, 2011

WANGARI MAATHAI IS NO MORE

Kenya's Nobel laureate and conservation heroine Professor Wangari Muta Maathai (aged 71), has died in Nairobi while undergoing cancer treatment.

"It is with great sadness that the Green Belt Movement announces the passing of its founder and chair, Professor Wangari Muta Maathai, after a long illness bravely borne," her organization said.

The environmentalist, activist and politician died at the Nairobi Hospital at around 10pm on Sunday (September 25th, 2011), according to officials at her Green Belt Movement organisation.

She was born on 1 April 1940 in Ihithe village, Tetu division, Nyeri District in Kenya. She was educated in the United States at Mount St. Scholastica and the University of Pittsburgh, as well as the University of Nairobi in Kenya.

Prof. Maathai won the Nobel Peace Prize in 2004 for promoting conservation, women's rights and transparent government - the first African woman to get the award.

She was elected as a Member of the Kenyan Parliament in 2002 and served as Assistant Minister for Environment and Natural Resources in the government of President Mwai Kibaki between January 2003 and November 2005.

In the 1970s, Maathai founded the Green Belt Movement, an environmental non-governmental organization focused on the planting of trees which has planted 20-30 million trees in Africa., environmental conservation, and women's rights. In 1984, she was awarded the Right Livelihood Award, and in 2004, she became the first African woman to receive the Nobel Peace Prize for “her contribution to sustainable development, democracy and peace.”
The organisation also campaigned on education, nutrition and other issues important to women.

Ms Maathai had been arrested several times for campaigning against deforestation in Africa.


source: http://www.wavuti.com/habari.html#ixzz1Z3n4cUFl

FATUMA KIMARIO SIO MUISLAMU- WAISLAMU TUNATUMIKA IGUNGA.

Naomba leo niandike jambo ambalo linawezekana kabisa kwa wengine wakaniona ama nimekuwa na msimamo tofauti kuhusu dini yangu tukufu ama labda wakafikiri kuwa na mimi nimeamua kuukana uislamu kwa manufaa ya wakristo na ama hata nimeamua kuwa mwanasiasa, jambo ambalo kati ya hayo hapo juu hakuna hata moja ambalo limenisukuma katika kuandika juu ya jambo hili leo.
Kilichonisukuma mpaka nikafikia kuandika makala haya ni kutokana na ukweli ambao nimeufahamu baada ya kutumia muda wangu kutafakari kuhusiana na malumbano ya siasa na dini ambayo yamekuwepo kwa mjuda mrefu na sasa yanaelekea kufikia kilele chake huko Igunga haswa juu ya “Ukristu wa CHADEMA” na “Uislamu wa CCM” NA CUF haijulikani kama wao ni waislamu ama ni wapagani kwani kwa sasa waislamu wameamua kuwa chama chetu kiwe ni CCM kitu ambacho sio sahihi na hakuna kikao wala mhadhara wowote ambao umewahi kufanyika na kufanya maamuzi hayo.Naandika kwa sababu ya picha ya leo ya gazeti la Tanzania Daima kuhusu hijabu na mtandio inafedhehesha uislamu na viongozi wetu mnadharaulika sasa kutokana na kutetea kitu ambacho ni fedheha sitaki muendelee .Fatuma Joseph Kimario sio Muislamu- (DC wa Igunga).
Ndugu zangu waislamu nimefanya utafiti na kugundua pasipo na shaka kuwa huyu dada yetu ambaye leo anatumiwa na CCM hata kuwafanya viongozi wetu wabadilishe maana halasi ya vazi la heshima la Hijabu kuwa ni kimtandio tuu ni kuwa sio muislamu kwa mujibu wa sheria za Allah mwenyewe.
Mama huyu ameolewa na bwana Joseph Kimario ambaye huyu Joseph ni mzaliwa wa Wilaya ya Rombo Kilimanjaro kutoka kijiji cha Olel, kata ya Makiidi na Tarafa ya Mkuu . Huyu mumewe kwa sasa anaishi Mbezi Beach jijini DSM na wanajenga nyumba nyingine Tegeta jijini DSM .
BWANA JOSEPH KIMARIO ni kiongozi wa dini ya kikatoliki katika parokia ya Mbezi –huyu ni mzee wa kanisa na ni mwenyekiti wa kigango cha mbezi kati sasa huyu ndio kaoa Muislamu kweli?Watoto wa Fatuma na Joseph wamebatizwa na ni wakatoliki isipokuwa mmoja wa kike ambaye mpaka sasa hajafanya maamuzi ila watoto wao ambao wanasoma na mmoja akiwa anasoma UDSM ni mwanakwaya katika kanisa katoliki chuo kikuuu.
Fatuma akiwa DSM hajawahi kukutwa kavaa hijabu hata siku moja na hata huko Igunga havai hijabu na ndio maana siku alipokutwa kava mtandio alikuwa kavaa sketi fupi ya kitenge na mtandio ule alivaa kwa sababu anaenda kukutana na wazee wa kiislamu huyu asitufanye tupoteze msimamo wetu kuna siku itakuwa aibu.
Ndoa yao bado nafuatilia ilifungwa wapi kwani taarifa hizi nimeweza kuzikusanya kwa muda huu ambao suala hili lilipoibuka na haswa nilipomsikia Safari akisema tufanye kwanza utafiti nikajua kuna kitu CDM wanajua na ndio maana wanajiamini na hata mwanazuoni Prof.Safari kuamua kutoa ufafanuzi.
Siku haya yakidhihirika waislamu tutaficha wapi nyuso zetu? Natoa tahadhari tuwe makini na kauli zetu.Mwenye ubishi kuhusiana na Uislamu wa Fatuma aje hapa na aseme kama mwanamke ambaye kaolewa na mkristu bado anakuwa na sifa ya uislamu ama laa na hata aina ya mifugo anayofuga Joseph kwenye shamba lake Tegeta inatia kinyaa na siwezi kuiandika hapa.
CCM inatutumia waislamu kwa manufaa yao Igunga.
Naomba nieleze ni kwanini sasa naamini kuwa waislamu tunataka kutumiwa na CCM kwa manufaa yao wenyewe ya kisiasa huku waislamu tukiendelea kuumizwa;1. Kitendo cha kumfukuza Rostam na kumlazimisha ajiuzulu ni wazi kuwa kilisukumwa na udini zaidi .Hii inatokana na ukweli kuwa alituhumiwa pamoja na wenzake wakristu wawili ambao ni Edward Lowassa na Andrea Chenge , ila aliyetakiwa kujiondoa ni Rostama tuu kwa kuwa ni muisilamu na kudhihirisha hilo CCM waliamua kuweka mgombea Mkristo Igunga ili kuongeza idadi ya wakristu bungeni kwa kuwapunguza waislamu.
2. CCM iliamua kumwondoa Muislam kutoka cheo cha katibu mkuu wa CCM ndugu Makamba na kumuweka mkatoliki Ndugu Wilson Mukama , ambaye juzi alitoa tuhuma nzito kwa nchi za kiislamu kama vile Pakistani, Afganistani na Libya .Hii ni dalili ya wazi kabisa kuwa Mukama anazo falsafa za kimarekeni kiuwa kila Muislamu ni gaidi kwanini asingesema kuwa Makomandoo wa CDM wametoka vatikani? CDM ina uhusiano gani na nchi za kiislamu?
3. Timu ya kampeni Igunga inaendeshwa na wakristu – hii ni kutokana na kuwa kuna ajenda ya kuongoza wakristu Bungeni na ndio maana sasa wanabebana wakristu kwa ajili ya kuhakikisha kuwa hilo linaweza kutimia hapa nawazungumzia wakina Mchemba,Mkapa,Mangula,Mashishanga . Hawa ni wakristu ambao wengine tangu 2005 hawakuwahi kuonekana wakifanya siasa ila leo ndio wapo Igunga kuongoza timu ya kampeni za CCM huku sisi waislamu tukitakiwa kutoa matamko ya kulaani CDM na kuisaidia CCM ambao wanajua wanatutumia tuu.
4. CCM ilikataa kumpitisha mgombea muislamu Igunga , huyu ni ndugu Jaffari ambaye anajulikana msimamo wake ulivyo dhabiti kwenye masuala ya Imani na huyu ndio angeweza kusimama kidete kuhakikisha kuwa waislamu tunapata mahakama ya kadhi kule Bungeni .Wameweka mkatoliki ambaye ikifika kupiga kura kuhusiana na jambo hilo imani yake itamsimamia zaidi.
5. Igunga inatumika kuuwa hoja ya kuandamana kuhusua mahakama ya kadhi. Tulitoa tamko kuhusiana na nia yetu ya kuandamana kudai mahakama yaq kadhi ili niwaambie ukweli ni kuwa viongozi wa dini 40 waliitwa na JK na kupatiwa kiasi cha shilingi milioni moja kila mmoja ili8 kui8zima hoja hii kwani ingemuweka pabaya na ndio maana leo Igunga inatumika kupoteza malengo ya waislamu na sisi tunajikuta tukiingia. Nina ushahidi kuhusiana na jambo hili na anayebisha aje hapa aseme japo kuuweka sasa ni kuwadhalilisha viongozi wangu wa dini .


MAANDALIZI YA MCHAKATO WA KATIBA MPYA .

Ndugu zangui waislamu tunagawanywa ili utakapoletwa mswada wa katiba mpya tugawanyike kwenye mambo yasiyokuwa ya msingi na kisha tufarakane na tushindwe kuingiza madai yetu ya kimsingi katika kuidai katiba mpya na haswa viongozi wetu wataendelea kutumiwa hivi hivi na sisi tukuendelea kukaa kimya basi kamwe hatutaweza kufanikiwa hata siku moja naomba tuamke kwani kuna mambo hayako sawa mimi niko kwenye mfumo ndio maana nawaambia kuwa tumetegwa na kama hatutaweza kujitanzua tutaangamia muda sio mrefu .
Baada ya kusema haya yote nawaomba viongozi wa Kiislamu tuchuinguze jambo hili kwani tutajikuta tunafikwa na aibu kuwa siku za usoni.Ni mimi mwana wenu.

Kuku Unaowafuga Mwenyewe Wanapokukataa! ( Makala, Raia Mwema)

 Na Maggid Mjengwa,

KUNA kisa cha bwana mfuga kuku aliyeshangazwa kwa kuku wake mwenyewe aliowafuga kumkataa. Alishangaa iweje kuku aliokuwa akiwapa pumba na mtama, wakala wakashiba, kisha waje wamwandame na hata kumparura.


Na mwanadamu unafanyaje unapofikwa na hali ya kuku wako unaowafuga mwenyewe kukukataa? Mwingine atajibu kwa haraka; ” nitawachinja!”
Hilo ni jibu la mtu mpumbavu; maana mwanadamu hafugi kuku ili awachinje wote kwa siku moja. Mbali ya kitoweo, anahitaji kuku wamtagie mayai na wamtotolee vifaranga wapya; hivyo basi, wamuinulie kipato chake.

Mwanadamu afanye nini basi?
Ndio, kwa mwanadamu, ukiona hata kuku wako unaowafuga wanakukataa, basi, kaa chini utafakari kwa kina. Kuna tatizo. Na tatizo si kuku, ni lako mfuga kuku. Yumkini banda la kuku unaowafuga halina madirisha ya kuwapa hewa na mwanga. Na siku zote, kuku hawabanani ila ni mwenye kuku ndiye anayewabana kuku wake. Na hata kuku hufikwa na ukomo wa kustahimili kubanwa.


Mwezi Februari mwaka huu niliandika katika safu yangu hii kuhusu kilichokuwa kikitokea katika nchi za Kiarabu ikiwamo Misri. Niliandika kuwa yanayotokea Misri na kwingineko iwe fundisho kwa Chama tawala Tanzania, CCM. Na nikasema kuwa mabadiliko yanakuja hata katika nchi zetu hizi, na kuwa tungeziona ishara.


Maana; tuliona kule Misri kuwa Wamisri wale walifikia ukomo wa uvumilivu wa kukandamizwa. Wakaingia mitaani kuandamana kwa mamilioni hata wakamtimua Hosni Mubarak madarakani.
Waarabu wale walikuwa na kiu ya uhuru, kiu ya haki . Ni kiu ya zaidi ya miongo mitano, miaka 50. Kule Misri, tuliwaona Wamisri wenye furaha kuu usiku ule wa mkesha wa ’Tahrir’; neno lenye maana ya ukombozi.


Wamisri walikesha wakiimba na hata kutoa machozi ya furaha. Misri, kama ilivyokuwa kwa Tunisia na juzi hapa Libya, hatukuziona bendera za vyama. Tulizoziona ni bendera za mataifa hayo.
Kwao, ilikuwa ni sawa na mataifa yao kuzaliwa upya. Niliandika kuwa, furaha ile ya Wamisri ni sawa kabisa na taifa lao kushinda kwa mara ya tano fainali za Kombe la Dunia.

Wamisri wale hawakuchoshwa tu na Hosni Mubarak. Walichoshwa na mfumo mzima na hususan chama chao tawala. Ndio, tulishuhudia, kuwa jengo la kwanza kutiwa kiberiti na waandamanaji lilikuwa ni jengo la Makao Makuu ya Chama tawala cha nchi hiyo cha NDP - National Democratic Party. Kilikuwa chama kikongwe na kilichoshika hatamu za uongozi.


Kwa Wamisri, NDP kilikuwa ni chama walichokihofia hata katika maisha yao ya kila siku. National Democratic Party kwa maana ya Chama Cha Taifa Cha Demokrasia hakikuwa cha Taifa na wala Demokrasia ndani yake. Kilikuwa chama cha wateule wachache akiwemo mwana wa Hosni Mubarak aitwaye Gamal Mubarak. Mwana huyu wa rais alipewa cheo cha ukatibu mkuu na aliandaliwa na baba yake kumrithi madaraka ya urais.


Ndio, Wamisri walifikia ukomo wa uvumilivu. Vijana wale wa Tunis, Cairo, Tripoli na Benghazi hawana tofauti na vijana wa Kigali, Nairobi, Dar es Salaam na Kampala. Tofauti ni kwenye viwango vya uvumilivu.
Ni kama kabati la nguo. Kabati likijaa nguo, na mwenye nalo akazidi kuweka nguo, basi, sio tu mwenye nalo atashindwa kulifunga, bali nguo zitaanza kuanguka.

Makabati ya vijana wa Tunisia , Misri na Libya yalishajaa. Ndio maana tumewaona vijana wale wakilala mbele ya vifaru vya jeshi . Walikuwa tayari kwa lolote liwalo na liwe. Makabati ya vijana wetu bado yana nafasi ya kuweka nguo. Busara kwa watawala wetu ni kutosubiri yajae.


Ndio, binadamu anayekandamizwa sana hufikia kikomo cha uvumilivu. Miaka kumi iliyopita hakuna aliyefikiri vijana wale wa Tunisia, Misri na Libya wangefanya waliyoyafanya.
Yaliyotokea Misri, Tunisia na Libya ni darasa kubwa kwa watawala na vyama barani Afrika kuwa unapoukandamiza mpira uliojaa na ukabonyea, basi, kuna matokeo ya upepo kupungua, mpira kufutuka upande mwingine au kupasuka. Mawili ya mwisho ni lazima yatokee, ni suala la wakati tu.


Viongozi Afrika wanapaswa kutambua sasa kuwa Mwafrika wa mwaka 1975 si Mwafrika wa mwaka 2011. Waafrika wameamka. Viongozi Afrika wana lazima ya kuendana na mabadiliko ya wakati. Hizi ni zama za mabadiliko. Na Mabadiliko ya amani Afrika yanawezekana, mwenye kuyazuia mabadiliko ya amani, atambue, kuwa mabadiliko yenye vurugu hayaepukiki. Hilo la mwisho lina hasara kubwa.

CCM ina cha kujifunza?
Ni ukweli, idadi ya Watanzania, na hususan vijana waliokichoka Chama tawala, Chama cha Mapinduzi inaongezeka kila kukicha. Kufikiri kingine ni kujidanganya. Leo kuna vijana wenye kiu kubwa ya kuiondoa CCM madarakani ili waone tu itakuwaje wakija wengine. Maana, CCM pia imejitengenezea mazingira ya kuhofiwa badala ya kuheshimiwa.


Mathalan, kuna wengi leo wananing’iniza bendera za CCM kwenye biashara zao au kujiita wana CCM si kwa sababu wanakipenda na kukiheshimu chama hicho; bali wanakihofia.
Ni ukweli leo kuna Watanzania wenye kukihofia zaidi Chama Cha Mapinduzi kuliko Mungu wanayemwabudu. Na lipi jema kwa mtawala na chama; kuhofiwa au kupendwa? Mwingine angependa vyote, lakini haiwezekani. Jema ni kupendwa na kuheshimiwa.


CCM itambue sasa kuwa, mabadiliko yanakuja hata Tanzania. Ni suala la wakati tu. Na vijana wa Tanzania huenda wasiingie mitaani wakafanya kama wenzao wa Misri, Tunisia na Libya. Watasubiri siku ile ya kwenda kupiga kura ifikapo 2015. Hilo la subira ya vijana ndilo tunaloliombea.


Na huku mitaani tunawasikia vijana wengi wa Kitanzania wenye kuisubiri kwa hamu 2015. Yumkini wamedhamiria kuandamana kwa wingi wakiwa na vitambulisho vyao vya kupigia kura. Wataandamana kwenda vituo vya kupigia kura kwa nia ya kuiondoa CCM madarakani kwa nguvu za kura.

Salama ya CCM?
Ni ukweli kuwa CCM ina hali ngumu kuelekea 2015. Chama kimepoteza mvuto kwa kundi kubwa la vijana. Anayesoma kwa makini alama za nyakati anaweza kuona kuwa CCM ikiwa na bahati inaweza kwa tabu kutoa rais 2015, lakini, takribani nusu ya wabunge wa bunge lijalo watatoka kambi ya upinzani. Na itakuwa miujiza kama rais wa 2020 atatoka CCM.


CCM ijiandae sasa kuwa chama cha upinzani. Na inaweza kubaki hai kwa muda mrefu kama itaipitisha nchi hii kwenye Katiba itakayoifanya Tanzania kuwa nchi ya kisasa zaidi. Yawepo mazingira ya uwezekano wa kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Maana; kwa Katiba ya sasa, CCM ikitoka madarakani, basi, yaweza pia ikawa ndio mwisho wake; maana chama hicho kitakufa.


Na CCM ya sasa inahitaji ‘Tahrir’ yake ya ndani ya chama. Nimepata kuandika kuwa ili CCM isalimike na kubaki madarakani katika chaguzi zijazo, sio tu inahitaji kufanya mabadiliko makubwa; bali mabadiliko makubwa yenye kishindo.


CCM inahitaji kurudi kwenye misingi iliyoanzisha chama hicho. Huu ni wakati wa kurudisha misingi ya kimaadili ya chama na uongozi. Misingi iliyokuwapo huko nyuma. Angalia, iko wapi Miiko ya Uongozi? Imevunjwa, na ndio maana ufisadi umetamalaki.


Kwa mwana CCM, sasa sio suala la kushinda uteuzi wa ndani ya Chama na kujihakikishia kuingia Ikulu au Bungeni, kuna umma unaotaka mabadiliko utakaomkabili mgombea wa CCM - awe mgombea urais, udiwani au ubunge. Kuingia ulingoni na ‘CCM ile ile’ itakuwa ni hatari kwa wagombea wengi wa CCM siku zijazo.


Ni ukweli, kuwa ndani ya CCM imeanza kuporomoka, misingi iliyopelekea kuanzishwa kwa Chama hicho tukianzia na vyama mama vya TANU na Afro- Shiraz. Hili ni jambo la hatari sana. Ikumbukwe, vyama mama kwa CCM, TANU na Afro- Shiraz, vilikuwa ni kimbilio la makabwela, kimbilio la wanyonge.


Lakini CCM ya sasa inakimbiliwa na wafanyabiashara, wasomi na wajanja wengine. Wasomi hapa kwa maana ya hata wale wenye taaluma zao. Wako tayari kuzikimbia taaluma zao na kuingia kwenye siasa za vyama, hususan Chama cha Mapinduzi. Baadhi yao wanasukumwa huko kwa ajili ya kutafuta maslahi zaidi. Maslahi binafsi. Na kuna wanaoambiwa; "Mkitaka mambo yenu yawanyokee, njooni CCM". Si mambo ya wananchi, ni mambo yao binafsi!


Kuna wanaokimbilia ndani ya CCM kwa kuamini katika malengo na madhumuni ya kuanzishwa kwa chama hicho. Lakini kuna wanaokimbilia ndani ya CCM wakiwa na malengo na madhumuni ya kwao binafsi yasiohusiana kabisa na ya CCM. Kwao wao, CCM ni sawa na daraja la miti la kuwasaidia kuvuka na kufika wanakotaka kwenda.


CCM ina nafasi ya kujisahihisha. Ianze kazi hiyo sasa. Nahitimisha.
MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo

HESABU YA VIBAKISHA CHADEMA,CCM NA CUF KATIKA KINYANG'ANYIRO-IGUNGA



Mgombea Ubunge Jimbo la Igunga kwa tiketi ya Cuf, Leopold Mahona (kulia) akicheza mchezo wa bao.
Daniel Mjema, Igunga

KAMPENI za uchaguzi mdogo jimbo la Igunga, leo zinaingia katika wiki ya lala salama huku tathmini ikionyesha kuwa mchuano mkali ni baina ya vyama vitatu, licha ya vyama nane kusimamisha wagombea wake.

Vyama vyenye ushawishi mkubwa kisiasa jimboni humo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2, ni CCM kilichomsimamisha Dk Dalaly Kafumu, CUF kilichomsimamisha Leopard Mahona na Chadema ambacho kimemsimaisha, Joseph Kashindye.

Uchaguzi huo pia unavishirikisha vyama vya SAU, UPDP, DP, AFP na Chausta, lakini baadhi yake kampeni zake zinaendeshwa kwa kusuasua, huku vingine vikishindwa kabisa kufanya kampeni hizo.

Katika muda wa wiki mbili za kampeni Igunga, kumekuwa na matukio baadhi ya vyama vinavyoshiriki uchaguzi huo kutuhumiana kwa matukio ya uhalifu, ukiwamokampeni chafu, ubakaji, kumwagiwa tindikali, udhalilishaji na hata vitisho vya kutumia silaha za moto kama bastola.

Mvutano mkali zaidi upo baina ya CCM na Chadema, ambavyo makada wake wamekuwa wakipiga kambi za muda mrefu, ikiwa ni pamoja na kulala katika maeneo yenye idadi kubwa ya wapigakura.

Juzi Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe ambaye ni miongoni mwa wanasiasa wenye ushawishi alitua kukiongezea nguvu chama chake, lakini tayari CCM kilikwishaongeza wapiga kampeni wake wakiwamo, Katibu Mkuu mstaafu wa chama hicho Philip Mangula. Kwa upande wake CUF kinajivunia mtaji wa kura 11,000 ilizopata katika uchaguzi wa mwaka jana.

Mbinu nyingine ambayo imekuwa ikitumiwa katika kampeni hizo ni wagombea kujinadi kwa lugha ya kisukuma kutokana na wapigakura wengi wa jimbo hilo kuzungumza lugha hiyo ikilinganishwa na Kiswahili.

Hali hiyo imekuwa ikiwapa wakati mgumu wanahabari kufuatilia mikutano hiyo kutokana na wengi kutofahamu lugha hiyo, isipokuwa pale anapokuwapo mkalimani wa kutafsiri maneno husika Kiswahili.

Katika wiki ya mwisho iyaoanza leo, viongozi wa kitaifa wa vyama vyenye ushindani, wanatarajiwa kuhamia Igunga, ili kunadi sera za wagombea wao ili kujihakikikisha ushindi.

Inachojivunia CCM
CCM ambacho kinadai kuwa na mtaji wa kura 39,000 ilizozipata katika uchaguzi mkuu uliomalizika Oktoba mwaka jana, kimekuwa kikijivunia mfumo wa uongozi kuanzia ngazi ya mabalozi, shina, kata hadi wilaya.

Chama hicho kinaamini kuwa kama viongozi wao hao hawatakisaliti basi kina uhakika wa kutetea kiti hicho kilichoachwa wazi na Rostam Aziz aliyejiuzulu huku kikiamini kushinda kwa zaidi ya asilimia 60.

Mbali na uongozi huo, lakini chama hicho kina madiwani 24 kati ya 26 na kinaamini kuwa madiwani hao pia wana ushawishi mkubwa kwa vile walichaguliwa na wananchi kwa kura.

Katibu Mkuu wa CCM, Willison Mukama wiki iliyopita alisema chama chake pia kinajivunia sera nzuri kwenye huduma za jamii ikiwamo mradi mkubwa wa maji wa Shinyanga-Nzega-Igunga ambao utafanya tatizo sugu la maji Igunga kuwa historia.

CCM kimejenga imani kwamba tuhuma dhidi ya Chadema kwamba wanafanya vurugu, zinaweza kukisadia kuendelea kuliongoza jimbo hilo ambalo halijapata kuwa na mwakilishi wa upinzani.

Baadhi ya makada wa CCM wanaweka wazi kwamba Chadema ambacho ni chama kikii cha upinzani nchini, kimejikuta kikisigana na CUF ambao pia ni wapinzani na kwamba CCM wanaweza kunufaishwa na hali hiyo.

Kwa mtizamo huo, CCM kinaamini CUF kitasaidia kupunguza kura za Chadema ambacho hakina mizizi jimboni humo ikilinganisha na CUF ambacho kilishiriki uchaguzi mkuu 2010 na kunyakua kura 11,000.

Hivyo ipo imani kwamba Chadema na CUF vinaweza kujikuta vikigawana kura za wale wanaounga mkono upinzani, hivyo CCM kushinda kwa urahisi.


Vijana kuwabeba Chadema

Kwa upande wake Chadema ambacho ni chama kipya katika siasa za Igunga, kinaamini kitashinda uchaguzi huo kwa kile kinachodai ni kufanikiwa kujipenyeza katika kundi la vijana ambao ni wengi.

Hakuna ubishi kwamba katika mikutano ya chama hicho, kundi kubwa linaloonekana kukiunga mkono ni vijana ambao wanaamini matatizo makubwa ya ajira na maisha magumu yamesababishwa na CCM.

Jambo jingine, Chadema kinaamini mgawanyiko ndani ya CCM uliosababishwa na kujiuzulu kwa Rostam, pia utapunguza kura za chama tawala na kuwanufaisha wapinzani.

Wafuasi wa Rostam wanadaiwa ‘kununa’ na kufanya kampeni za chinichini ili kuhakikisha CCM hakishindi uchaguzi huo.

Jambo lingine ambalo Chadema kinaamini litapunguza kura za CCM ni hatua ya kumsimamisha Dk Kafumu katika wakati ambao kuna kelele nyingi kuhusu ufisadi katika sekta ya madini ambayo yanadaiwa kutowanufaisha Watanzania.

Kabla ya kuteuliwa kwake kupeperusha bendera ya CCM, Dk Kafumu alikuwa kamishina wa madini na Chadema na CUF vinatumia hilo kama silaha ya kummaliza mgombea huyo kwamba alishiriki ufisadi.

CUF na mtaji wa kura 11,000
CUF kwa upande wao wanaamini kuwa kura 11,000 kilizozipata 2010, mgawanyiko ndani ya CCM unaotokana na kundi la Rostam na vurugu zinazotokea jimboni humo zitasaidia kukivusha na kushinda.

Mbali na hayo lakini CUF kinaamini kuwa ndicho pekee kimeendesha kampeni za kistaarabu kulinganisha na vyama vingine na kutokana na hulka ya wenyeji kutoshabikia vurugu basi watakipa kura.

Pia CUF kinaamini kwamba mchuano mkali kati ya Chadema na CCM kutavifanya vyama hivyo viwili kugawana kura hivyo wao kupata ushindi kutokana na ushawishi walioufanya kwenye kampeni.

CUF kinaamini mgombea wake ndiye mwenye nguvu na anayekubalika zaidi na kwamba hata 2010 angeweza kuibuka mshindi lakini kutokana na ‘nguvu’ kubwa aliyoitumia Rostam ndio iliyochangia kumwangusha.

Kinachotarajiwa

Kutokana na hali ilivyo na ushindani mkubwa baina ya vyama vya Chadema, CUF na CCM, wadadisi wa siasa wanasema lolote linaweza kutokea katika jimbo hilo.

Wiki ya mwisho ya kampeni hizi inaweza kutoa mwelekeo wa nani atakuwa mshindi lakini kwa mtizamo wa kidadisi, hadi sasa hakuna chama chochote chenye uhakika wa ushindi.

Uchaguzi huo mdogo unatarajiwa kufanyika Oktoba 2 huku wapiga kura waliojiandikisha wakiwa 170,000 lakini wanaweza wasijitokeze wote kama ilivyotokea mwaka jana ambapo ni asilimia 40 waliojitokeza.


Sunday, September 25, 2011

Zitto afunika IGUNGA

Mtani wangu Aden,achana na bastola,rudi kwenye jambia

 
Mtani wangu Aden Rage,

Hivi tangu lini Mnyamwezi wa Urambo akabeba bastola kiunoni? Na unafanyaje bastola inapoishiwa risasi? Yaweza kuwa mauti yako.  Tuliopitia jeshini tunajua  kuwa kuna silaha zenye singe. Bastola haina singe.

Rage achana na bastola, rudi kwenye jambia, silaha yetu ya jadi. Na kwenye mapambano ya ana kwa ana na hususan mtu kwa mtu , jambia ndio silaha ya uhakika. Na pambano la kutumia jambia lina hatua mbili; mosi, kumshambulia adui kwa kutumia ubapa wa jambia. Pili, ikitokea pambano likawa gumu na hata adui akakamata jambia, basi, mara tu jambia likiwa mikononi mwa adui, unachotakiwa ni kuchomoa sime na kumwacha adui akiwa amebaki na mfuko wa sime.

Na mapambano mengi Afrika hayafikii mtu akachomoa sime!
Sasa mtani wangu Aden,  iweje umeamua kuwatisha Wanyamwezi wenzako kwa bastola?

Any way, yumkini Aden Rage lilikuwa jina maarufu sana pale klabuni kwetu Simba Sports Club,  Msimbazi, Kariakoo. Leo  umaarufu wa Mnyamwezi wa Urambo Aden Rage umeenea Unyamwezizi na Usukumani kote,  na ukafika mpaka Manyema ya Kigoma. Kisa? Bastola kiunoni. Wanyamwezi bure kabisa!

Maggid,
Iringa,
Septemba 24, 2011


source: http://www.wavuti.com/habari.html#ixzz1YyTtvHA2

Saturday, September 24, 2011

Madiwani CCM, Chadema Songea wazipiga kavukavu

KATIKA hali isiyo ya kawaida, Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma, wamerushiana makonde na kusababisha uchaguzi wa meya kuvunjika.
Hatua hiyo ilitokana na baada ya Naibu meya wa halmashauri hiyo, Mariam Dizumba, kudaiwa kuiba kura zilizopigwa na madiwani hao kwenye uchaguzi wa kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Meya wa halmashauri hiyo, Ally Manya, aliyefariki dunia miezi michache iliyopita.

Kutokana na mapigano hayo baadhi ya madiwani walijikuta wakijeruhiwa na wengine kupoteza simu na vitu vya thamani.Katika uchaguzi huo, ulioanza kwa malumbano makali yaliyodumu kwa zaidi ya dakika 20 kati ya madiwani wa Chadema na wenzao wa CCM, ambao walikuwa wanajadili jinsi uchaguzi huo utakavyokuwa huru na haki kutokana na upinzani kutosimamisha mgombea.

Kutokana na hali hiyo, Msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Nachoa Zakaria, alitoa ufafanuzi wa kanuni za uchaguzi wa nafasi hiyo, huku akiwataka kupiga kura za ndiyo au hapana na kwamba, wapiga kura halali waliojiorodhesha ni 26, akiwamo na Mbunge wa Songea Mjini, Dk Emmanuel Nchimbi.

Baada ya hali hiyo kutulia, Zakaria aliita orodha ya wajumbe na kuwataka kuchukua karatasi za kupigia kura, madiwani wote walipiga kura na kuitwa kuzihesabu.

Zoezi la hesabu lilipomalizika, Naibu meya Dizumba alilisimama na kuanza kutangaza matokeo, akitaja mgombea pekee wa CCM, Charles Mhagama, alipigiwa kura za ndiyo 14 na hapana 12.

Dizumba alisema kutokana na matokeo hayo, Mhagama ndiye meya mpya wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea.“Naomba msimamizi wa uchaguzi umwite Diwani Mhagama avae joho la Umeya na kukalia kiti chake,” alisema Dizumba.
Baada ya Msimamizi kumwita Mhagama na kumtaka kuvaa joho la Umeya, baadhi ya madiwani walimtaka msimamizi kuhesabu upya kura hizo ili madiwani wote washuhudie.

“Naomba msimamizi usitishe zoezi la kumtaka Diwani Mhagama akalie kiti cha Umeya, kwa sababu kuna mashaka makubwa na zoezi la utangazaji matokeo, hivyo zihesabiwe kura upya na madiwani wote wazione,” alisema Diwani wa Kata ya Mfaranyaki, Seneta Yatembo.

Wakati wakiendelea kuzozana, Diwani wa Viti Maalum (Chadema), Rhoda Komba, akawaita madiwani wenzake kushuhudia Dizumba alivyokuwa anaiba kura zilizopigwa za hapana kutoka kwenye sanduku la kura, huku akichukua kura za ndiyo kutoka kwenye mkoba wake kuziweka ndani ya sanduku.

Hali hiyo ilisababisha vurugu kubwa na kumfanya Dk Nchimbi (ambaye ni WAZIRI wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo) kukimbia na sanduku la kura kuelekea nje ya ukumbi, kabla ya kunyang’anywa na kutakiwa kulirudisha ndani na madiwani wakiongozwa na wenzao wa Chadema.

Baada ya tafrani hiyo, madiwani wa Chadema waliitisha kikao na waandishi wa habari na kutoa tamko la kutomtambua Mhagama kuwa meya na kwamba, wameomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), kuitisha uchaguzi mwingine. Chadema ina madiwani saba na CCM 20.

Kwa upande wa madiwani wa CCM, walisema walichofanya wenzao wa Chadema kwa kufanya fujo na kutaka kuwapiga wengine ni kitendo kibaya, kukuza demokrasia.
SOURCE:Mwananchi

Friday, September 23, 2011

PICHA INAYOLETA GUMZO

 
kikwete 50 cent
SOURCE:WAVUTI

MIKATABA INAVYOSAINIWA


Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe (mwenye furana ya njano kati )
akiwa na viongozi wa wadau mbali mbali wa Ludewa
baada ya kumaliza hafla fupi ya kusaini mkataba huo.






Nakumbuka mwaka huu katika kikao cha Bunge, ndani ya bunge au nje ya bunge, Mhesh. Deo F. Haule Mbunge wa Ludewa alipata kutamka kwamba Katibu wa Wizara ya madini David Jairo alikuwa kizuio cha kusaini mkataba wa mradi wa madini Ludewa.

Kwenye habari hiyo hapo chini:
Akizungumza na waandishi wa habari,
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya NDC Bwana Mzindakaya alisema, kuna watanzania wenzetu ambao wanafanya kila jitihada ili kuhakikisha mradi huo unakwama lakini yeye amesema hakuna mtu tena atakayediriki kuuzuia mradi huo usianze kwani huo ni mradi wa Taifa
Baada ya Jairo kuwekwa mahabusu ya nje, mradi wa Makaa ya mawe na chuma Ludewa umeenda chapuchapu na kusainiwa. Je Jairo alikuwa kizuio? Jairo ana mfumo dume wa kujali maendeleo ukanda aliotoka tu na kutojali maendeleo kitaifa?

Subira yavuta heri ama hayawi hayawi sasa yamekuwa ndivyo wanavyoweza kusema wakazi wa wilaya ya Ludewa mkoa wa Iringa ama mkoa mpya wa Njombe baada ya Ule mradi ambao ulionekana kuwa ni ndoto ya mchana, mradi wa makaa ya mawe wa Mchuchuma na Mradi wa Chuma wa Liganga utaanza muda wowote baada ya kusainiwa leo mchana.

Akithibitisha baada ya kushuhudia tukio hilo, Mbunge wa Ludewa Mhe. Deo Filikunjombe amesama leo LUDEWA IMEPATA UHURU. Miaka nenda rudi ilikuwa ni historian a maelezo mengi tu kuhusu Miradi hiyo miwili lakini leo Mkurugenzi wa bodi ya Wakurugenzi wa National Development Corporation NDC Bwana Chrisant Mzindakaya amesaini kwa niaba ya serikali na mwakilishi wa kampuni Liu Canglong alisaini kwa niaba ya kampuni ya Hongda Group ya China.

Mradi wa Liganga una chuma kiasi cha tani 1.2 bilioni na utaanza kuzalisha tani milioni tatu kwa mwaka na mradi wa mchuchuma utakuwa na uwezo wa kutoa tani milioni tatu za chuma kwa mwaka. Mradi wa Mchuchuma una kiasi cha tani 400 milioni za makaa yam awe ambayo yanaweza kuchimbwa kwa zaidi ya miaka 500. Kabla ya kuanza miradi hiyo, Mzindakaya alisema itachukua hadi miezi sita ili kuhakiki na kutathmini thamani halisi ya makaa ya mawe na itahitajika miezi hadi 36 kutathmini chuma ghafi huko Mchuchuma na Liganga.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi baada ya kusainiwa mkataba huo, Mbunge wa Ludewa Mhe. Deo Filikunjombe alisema, licha ya faida zitakazotokana na hisa za serikali ambazo kwa awamu ya kwanza zitakuwa 20%, kutakuwa na faida nyingine lukuki zikijumuisha, maendeleo ya viwanda vidogo vidogo, viwanda vya chuma, ujenzi wa miundo mbinu ya reli, barabara ya lami, mfumo wa kusafirishia umeme, bandari, viwanja vya ndege na makazi ya watu. Kuhusu mapato ya serikali Mhe. Filikunjombe alisema, kutakuwa na mapato ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 1.2 au shilingi za Kitanzania takribani trilioni 2 zitakazotokana mauzo ya mazao ya chuma na umeme kwa mwaka. Hivyo inatarajiw serikali itapata mapato mengi kupitia kodi mbalimbali.

Mradi utakuwa unaajiri wafanyakazi 8000 kila mwaka na mradi wa umeme utaanza kutoa umeme wa MGW 600 ambazo zitatengenezwa kwa namna ambayo itakuwa ni rahisi kuuongeza nguvu na kutengeneza MGW zitakazohitajika na Taifa.
Sherehe hizo zilihudhuriwa na Makamu wa Rais, Mhe. Ghalib Bilal ambaye alikuwa mgeni Rasmi pamoja na viongozi wengine wa chama, serikali, vyama vya siasa, wazee wawakilishi kutoka Ludewa, Mkuu wa wilaya ya Ludewa Mhe. Na viongozi wengine kutoka wilaya ya Ludewa. Kulikuwa vile vile na wawakilishi kutoka kampuni ya Hongdan Group waliokuja na ndege mbili kutoka China pamoja na wadau wengine wa miradi hiyo ya Maendeleo.

Habari zaidi kuhusu namna Taifa litakavyofaidika na miradi hiyo zitatolewa baada ya muda si mrefu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya NDC Bwana Mzindakaya alisema, kuna watanzania wenzetu ambao wanafanya kila jitihada ili kuhakikisha mradi huo unakwama lakini yeye amesema hakuna mtu tena atakayediriki kuuzuia mradi huo usianze kwani huo ni mradi wa Taifa.

SHAHADA ZA KURA-IGUNGA

Picture
Picture
SOURCE;www.wavuti.com

TIGO YAIPA SHULE YA MSINGI TUANGOMA VITABU

Kampuni ya simu za mikononi ya Tigo kwa kupitia kampeni yake ya “Tigo tuChange” imetoa msaada wa vitabu vya kiada na ziada kwa shule ya msingi Tuangoma iliyopo manispaa ya temeke ikiwa ni moja kati ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na kampuni hii katika kuchangia sekta ya elimu ili kuongeza kiwango cha ufaulu nchini.
Picture
Shule ya msingi  Toangoma ya jijini DSM ni moja kati ya shule za msingi mbalimbali nchini zitakazofaidika na kampeni hii ya “Tigo tuChange” ambapo hivi karibuni vitabu vitasambazwa katika mikoa ya Tabora, Kagera na Mtwara.

Akielezea madhumuni ya kampeni ya Tigo Tuchange wakati wa kukabidhi vitabu katika shule hiyo,  mwanasheria wa kampuni ya MIC – TIGO TUMAINI SEKWA SHIJA amesema Tigo kwa namna ya pekee imeguswa na matatizo yanayozikumba shule mbalimbali za msing na yamekuwa kikwazo kikubwa katika kuongeza kiwango cha elimu nchini ndio maana baada ya kutoa vibao vya mapajani kwa wingi katika shule mbalimbali sasa ni ni vitabu.

SHIJA ameongeza kuwa uzalendo wa watanzania na hasa katika kuipenda tigo umetoa msukumo wa wao kurudisha sehemu ya faida kwa jamii, ‘watanzania wameendelea kuwa msaada mkubwa kwetu na wameendelea kutuunga mkono siku zote sasa na sisi kwanamna ya pekee hasa ukizingatia kuwa Tigo ni sehemu ya watanzania hatuna budi kurudisha sehemu ya kile tunachokipata kwa jamii inayotuunga mkono siku zote.’
Picture
Mkurugenzi wa Mamlaka ya elimu Tanzania ROSEMARY LULABUKA amesema anafurahia jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tigo katika kusaidia sekta ya elimu.

‘Hatua hii ni nzuri na yenye manufaa kwa Taifa kwani vitabu vimeendelea kuwa tatizo kubwa katika sehemu mbalmbali ndani ya nchi na hivyo tunaishukuru tigo kwa kutufuata na kutaka ushiriki wetu katika kampeni hii na tungependa mashirika na taasisi binafsi na za serikali kuiga mfano huu wa Tigo katika kuchangia elimu ili tuweze kuhakikisha watoto wanapata nyezo muhimu za kujifunzia wakiwa shuleni” 
Picture
SHIJA amesema kuwa jumla ya shilingi 25,930,160 zilipatikana katika program maalum ya Tigo Tuchange iliyofanyika tarehe 9 mwezi wa saba 2011 kuanzia saa tatu mpaka saa nne asubuhi ambapo ndani ya muda huo mteja yeyote wa Tigo aliyenunua muda wa maongezi wa kuanzia shilingi mia tano na kuendelea alichangia kupatikana kwa fedha hizo ambazo ndizo zimetumka katika kununulia vitabu hivyo ambavyo vitatolewa kwa shule za msingi kwa kupitia mwongozo unaotolewa na mamlaka ya elimu Tanzania.

Diwani wa Kata ya Chang'ombe afariki Dunia-Dodoma

Juzi tarehe 21/9 aliyekuwa diwani wa kata ya Chang'ombe kupitia tiketi ya CCM amefariki dunia. Tukio hili limetokea wakati bado kuna hekaheka za uchaguzi mdogo katika kata ya Kikuyu kusini na tarehe ya uchaguzi ni tarehe 2/10, uchaguz huu unafanyika kutokana na aliyekua diwani wa kata hiyo (kikuyu kusini) kufariki dunia mwezi Aprili.

Mungu azilaze mahali pema peponi roho za marehemu. Amina

UPINZANIA ZAMBIA HATIMAYE WAMECHUKUA NCHI

Nimekua nikifuatilia kwa karibu uchaguzi wa Jirani zangu na Wakwe zangu hapo Zambia, hatimae Upinzani wamechukua nchi na hio ndio ishara Nzuri kwamba sasa wanaaminiwa na harakati za Kuapishana ndio zinakamilika hivyo. Lazima jamaa watavunja Tume ya Uchaguzi iliyochelewesha matokeo; hii ndio spech ya Ya rais aliyeshindwa.
I HAVE CALLED THIS PRESS CONFERENCE TO SAY A FEW WORDS. THE ELECTION CAMPAIGN OF 2011 IS OVER. THE PEOPLE OF ZAMBIA HAVE SPOKEN AND WE MUST ALL LISTEN. SOME WILL BE HAPPY WITH WHAT THEY HAVE HEARD, OTHERS WILL NOT.
THE TIME NOW IS FOR MATURITY, FOR COMPOSURE AND FOR COMPASSION. TO THE VICTORS, I SAY THIS: YOU HAVE THE RIGHT TO CELEBRATE BUT DO SO WITH A MAGNANIMOUS HEART. ENJOY THE HOUR BUT REMEMBER THAT A TERM OF GOVERNMENT IS FOR YEARS.
REMEMBER THAT THE NEXT ELECTION WILL JUDGE YOU ALSO.
TREAT THOSE WHO YOU HAVE VANQUISHED WITH THE RESPECT AND HUMILITY THAT YOU WOULD EXPECT IN YOUR OWN HOUR OF DEFEAT.

I KNOW THAT ALL ZAMBIANS WILL EXPECT SUCH BEHAVIOUR AND I HOPE IT WILL BE DELIVERED. SPEAKING FOR MYSELF AND MY PARTY, WE WILL ACCEPT THE RESULTS. WE ARE A DEMOCRATIC PARTY AND WE KNOW NO OTHER WAY.
IT IS NOT FOR US TO DENY THE ZAMBIAN PEOPLE. WE NEVER RIGGED, WE NEVER CHEATED, WE NEVER KNOWINGLY ABUSED STATE FUNDS. WE SIMPLY DID WHAT WE THOUGHT WAS BEST FOR ZAMBIA. I HOPE THE NEXT GOVERNMENT WILL ACT LIKEWISE IN YEARS TO COME.
ZAMBIA DESERVES A DECENT DEMOCRATIC PROCESS. INDEED, ZAMBIA MUST BUILD ON HER PAST VICTORIES. OUR INDEPENDENCE WAS HARD WON, OUR DEMOCRACY SECURED WITH BLOOD.
ZAMBIA MUST NOT GO BACKWARDS, WE MUST ALL FACE THE FUTURE AND GO FORWARD AS ONE NATION. NOT TO DO SO WOULD DISHONOUR OUR HISTORY.
TO MY PARTY, TO THE MMD CANDIDATES WHO DID NOT WIN, THE LESSON IS SIMPLE. NEXT TIME WE MUST TRY HARDER.
WE FOUGHT A GOOD CAMPAIGN. IT WAS DISCIPLINED. I STILL BELIEVE WE HAD A GOOD MESSAGE AND WE REACHED EVERY PART OF THE COUNTRY.

WE TRAVELLED TO ALL NINE PROVINCES AND WE SPOKE TO ALL ZAMBIANS. TO THOSE WHO WORKED EVERY HOUR OF THE DAY, I SAY ‘THANK YOU’. YOU HAVE DONE YOUR BEST. BUT, SADLY, SOMETIMES OUR BEST IS NOT GOOD ENOUGH.
DO NOT BE DISHEARTENED. THE MMD WILL BE BACK. WE MUST ALL FACE THE REALITY THAT SOMETIMES IT IS TIME FOR CHANGE. SINCE 1991, THE MMD HAS BEEN IN POWER. I BELIEVE WE HAVE DONE A GOOD JOB ON BEHALF OF ALL ZAMBIANS.
FREDERICK CHILUBA LED US TO A GENUINE MULTI-PARTY STATE AND INTRODUCED THE PRIVATE SECTOR TO OUR KEY INDUSTRIES. ZAMBIA WAS LIBERATED BY AN MMD IDEAL BUT MAYBE WE BECAME COMPLACENT WITH OUR IDEALS. MAYBE WE DID NOT LISTEN, MAYBE WE DID NOT HEAR.
DID WE BECOME GREY AND LACKING IN IDEAS? DID WE LOSE MOMENTUM? OUR DUTY NOW IS TO GO AWAY AND REFLECT ON ANY MISTAKES WE MAY HAVE MADE AND LEARN FROM THEM. IF WE DO NOT, WE DO NOT DESERVE TO CONTEST POWER AGAIN.
THE ZAMBIA WE KNOW TODAY WAS BUILT BY AN MMD GOVERNMENT. WE KNOW OUR PLACE IN HISTORY AND WE KNOW THAT WE CAN COME BACK TO LEAD AGAIN IN THE FUTURE. A NEW LEADERSHIP WILL BE CHOSEN, AND THAT LEADERSHIP WILL BE FROM THE YOUNGER GENERATION.
MY GENERATION… THE GENERATION OF THE INDEPENDENCE STRUGGLE– MUST NOW GIVE WAY TO NEW IDEAS; IDEAS FOR THE 21ST CENTURY. FROM THIS DEFEAT, A NEW, YOUNGER MMD WILL BE RE-BORN. IF I CAN SERVE THAT RE-BUILDING, THEN I WILL.
I MUST THANK MY CABINET FOR DELIVERING ON OUR PROMISES. WE DID A LOT OF GOOD FOR ZAMBIA. MANY OF OUR PROJECTS WILL BLOSSOM INTO BRIGHT FLOWERS. SOME OF YOU WILL BE BACK TO SERVE ZAMBIA AGAIN – I KNOW YOU WILL DO YOUR BEST FOR YOUR PARTY AND FOR YOUR COUNTRY.
TO THE CIVIL SERVANTS AND GOVERNMENT OFFICIALS, IT HAS BEEN A PRIVILEGE TO SERVE WITH YOU. WE HAVE WORKED MANY LONG HOURS TOGETHER. WE DID IT NOT FOR OURSELVES BUT FOR ZAMBIA. SERVE YOUR NEXT MASTERS AS YOU DID ME, AND ZAMBIA WILL BE IN GOOD HANDS.

I MUST THANK MY FAMILY AND MY WIFE. THEY HAVE STOOD BY ME AND I CANNOT ASK FOR MORE LOYALTY THAN THAT WHICH THEY HAVE DISPLAYED. I LOVE YOU ALL DEARLY AND I WILL ALWAYS BE IN YOUR DEBT.
BEING PRESIDENT IS HARD WORK, IT TAKES LONG HOURS OF WORK. AND BECAUSE OF IT, I HAVE NOT ALWAYS BEEN THERE FOR YOU. YET, STILL YOU WERE THERE FOR ME.
WORDS CANNOT EXPRESS THE DEPTH OF MY LOVE FOR YOU ALL. ALL I ASK IS THAT MY FAMILY CONTINUES TO SERVE ZAMBIA AS I HAVE SOUGHT TO DO.
BUT MY GREATEST THANKS MUST GO TO THE ZAMBIAN PEOPLE. WE MAY BE A SMALL COUNTRY ON THE MIDDLE OF AFRICA BUT WE ARE A GREAT NATION. SERVING YOU HAS BEEN A PLEASURE AND AN HONOUR. I WISH I COULD HAVE DONE MORE, I WISH I HAD MORE TIME TO GIVE.
OUR POTENTIAL IS GREAT. OUR RESOURCES ARE IMPRESSIVE.
I URGE YOU ALL NOW TO RALLY BEHIND YOUR NEW PRESIDENT.
YES, WE MAY HAVE DIFFERENT IDEAS BUT WE BOTH WANT THE SAME THING – A BETTER ZAMBIA.

NOW IS NOT THE TIME FOR VIOLENCE AND RETRIBUTION.
NOW IS THE TIME TO UNITE AND BUILD TOMORROW’S ZAMBIA TOGETHER. ONLY BY WORKING TOGETHER CAN WE ACHIEVE A MORE PROSPEROUS ZAMBIA.

IN MY YEARS OF RETIREMENT, I HOPE TO WATCH ZAMBIA GROW. I GENUINELY WANT ZAMBIA TO FLOURISH. WE SHOULD ALL WANT ZAMBIA TO FLOURISH. SO, I CONGRATULATE MICHAEL SATA ON HIS VICTORY.
I HAVE NO ILL FEELING IN MY HEART, THERE IS NO MALICE IN MY WORDS. I WISH HIM WELL IN HIS YEARS AS PRESIDENT.
I PRAY HIS POLICIES WILL BEAR FRUIT.

BUT NOW IT IS TIME FOR ME TO STEP ASIDE. NOW IS THE TIME FOR A NEW LEADER. MY TIME IS DONE. IT IS TIME FOR ME TO SAY ‘GOOD BYE’.
MAY GOD WATCH OVER THE ZAMBIAN PEOPLE AND MAY HE BLESS OUR BEAUTIFUL NATION.
I THANK YOU.


Zambia: Presidident Rupiah Banda Bids Farewell to Zambians | LusakaTimes.com na Aljazeera

Thursday, September 22, 2011

Soko kuu la kibakwe

CHADEMA 74%-IGUNGA

•  Kapteni Komba, Mukama nusura washikane mashati

na Mwandishi wetu
WAKATI zikiwa zimesalia wiki takriban mbili kabla ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga, timu ya kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) imesambaratika, Tanzania Daima Jumatano limebaini.
Wakati CCM ikisambaratika, tathmini ya awali ya uchaguzi iliyofanywa jimboni humo, inaonyesha kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kitaibuka na ushindi wa zaidi ya asilimia 74 ya kura zote.
Tathmini hiyo ambayo imefanywa na CHADEMA kwa kuwashirikisha wanazuoni na baadhi ya wanahabari kwa takriban wiki tatu, imetumia takwimu za maeneo ya vijijini na mjini Igunga.
Habari zaidi zinasema CHADEMA imefanya uchambuzi na kuweka mikakati makini ya kudhibiti mianya yote ya hujuma, kwa kuwatumia makada wake na baadhi ya wana CCM na wananchi wanaojitolea, wasioridhishwa na mwenendo wa jumla wa chama tawala jimboni humo.
Nguvu hiyo ya CHADEMA ndiyo imesababisha baadhi ya wanachama na makada wa CCM kuvujisha taarifa za hujuma zilizomhusisha Mkuu wa Wilaya, Fatuma Kimario, na mabalozi wa nyumba 10 waliokamatwa na vijana wa CHADEMA na kuwekwa chini ya ulinzi.
Baadhi ya makada maarufu wa CCM wanasema wameshakata tamaa na kwamba mbinu pekee inayoweza kukiwezesha chama chao kushinda ni nguvu ya dola; si sanduku la kura.
Hata hivyo, walionyesha wasiwasi kwamba jinsi CHADEMA walivyojiandaa, hata hizo nguvu za dola zinaweza zisifue dafu, kwani makundi yaliyo ndani ya CCM ndiyo yanayoelekea kukiongezea CHADEMA nguvu na kukipa ushindi.
Habari zaidi kutoka Igunga ambako kampeni za vyama vya siasa zimeshika kasi, zinasema kuwa timu ya kampeni iliyokuwa ikiongozwa na Mbunge wa Iramba Mashariki, Mwigulu Mchemba, imesambaratika hasa baada ya Mchemba kukumbwa na kashfa ya fumanizi na mke wa kada mwenzake wa CCM.
Habari kutoka ndani ya CCM Igunga na Ofisi Ndogo ya Makao Makuu jijini Dar es Salaam, zilisema kuwa kuna shinikizo kutoka ndani ya chama hicho kutaka Mchemba aondolewe kwenye kampeni hizo, kwa madai kuwa kashfa ya fumanizi inaweza kuwavurugia kampeni zao.
Kwa mujibu wa habari hizo, tangu kuibuka kwa kashfa hiyo, timu ya kampeni ya CCM imegawanyika.
Wapo wanaotaka Mchemba aondolewe kwenye kampeni, lakini pia wapo wanaotaka aendelee.
Kusambaratika kwa timu hiyo ya kampeni kumetokana na uchunguzi wa CCM wa hivi karibuni ambao ulibaini kuwa timu hiyo haiko kitu kimoja.
“Timu yetu ya kampeni Igunga haiko kitu kimoja, na hata taarifa za kashfa ya kuwa meneja wetu wa kampeni ana uhusiano usiofaa na mke wa kada mwenzake wa CCM, zilisambazwa na kundi la vijana wa CCM wasiotaka jimbo hilo libaki CCM,” kilisema chanzo chetu cha habari.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, CCM inaamini kuwa kundi hilo lililoasi ndani ya CCM, lilipanga mkakati huo na kuhakikisha kigogo huyo wa CCM ananaswa na kukisababishia chama hicho kukosa ushindi.
Duru za siasa kutoka ndani ya CCM, zinasema kuwa inashangazwa na kila mkakati unaofanywa kwa siri na chama hicho, umekuwa ukinaswa na wapinzani wao katika mazingira ambayo wanaendelea kuyafanyia utafiti ili kuwaengua baadhi ya wajumbe walioko ndani ya timu ya kampeni.
Wiki iliyopita, timu hiyo ya kampeni ya CCM, iliingia katika msukosuko mkubwa baada ya Mwingulu, anayeongoza kampeni hiyo, kudaiwa kufumaniwa na mke wa mtu.
Inadaiwa kuwa sakata hilo lilianza baada ya mume wa mwanamke anayedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kigogo huyo kuvamia chumba ambacho watuhumiwa hao walikuwamo na kuanza kumwadhibu mkewe kwa kipigo.
Wakati vuta nikuvute kati ya mke na mume ikiendelea chumbani, kigogo huyo wa CCM alifanikiwa kutoroka na kuwaacha wanandoa hao ambao wote wawili ni makada wa CCM, wakiendelea kupambana.
Mtafaruku huo ulimsababishia mwanamke huyo aliyekuwa miongoni mwa kundi la mabinti wapatao 10 wanaotumika kuhamasisha kwenye kampeni hizo kupata majeraha makubwa yaliyomlazimisha apelekwe hospitalini kwa ajili ya matibabu.
Kabla ya kwenda hospitalini, mwanamke huyo alilazimika kupita katika kituo cha polisi cha Igunga ili akapatiwe fomu maalum ya idhini ya matibabu (PF3).
Wakati nje ya uwanja wa kampeni mambo yakiwa hivyo, CCM mwishoni mwa wiki ilikuwa na kikao maalum kilichoongozwa na Katibu Mkuu, Willson Mukama, kufanya tathmini ya namna kampeni zao zinavyoendeshwa na mbinu za kukabiliana na wapinzani wao, hasa CHADEMA, ambao wameonekana kuwa na mvuto zaidi.
Wajumbe wengine waliokuwa kwenye kikao hicho ni baadhi ya wajumbe wa sekretarieti, pamoja na aliyekuwa Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Philip Mangula, na kiongozi wa kundi la sanaa za maonyeshola la CCM la Tanzania One Theatre (ToT), Kapteni John Komba.
Habari ndani ya kikao hicho, zilisema kuwa kilikuwa na mvutano mkubwa hasa kati ya Kapteni Komba na Mukama kuhusu namna ya kuendesha kampeni hizo.
“Kapteni Komba aliwasilisha taarifa yake ya kutaka aongezewe fedha kwenye kundi lake la ToT, tofauti na fedha wanazolipwa sasa ambazo alisema hazitoshi, Katibu Mkuu alikuwa hataki kuongeza hata senti tano. Hapo palikuwa hapatoshi. Mzozo ulikuwa mkali sana,” alisema mmoja wa wajumbe wa kikao hicho mjini Igunga.
Habari hizo zilizema kuwa mzozo huo ulimalizwa na Mangula ambaye naye ameletwa mjini hapa kuimarisha kampeni za CCM ambazo tathmini iliyofanywa ndani ya chama hicho inaonyesha kuwa wanaweza kushindwa vibaya kwenye uchaguzi huo.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa kundi la TOT, lina hali mbaya kifedha na hivi sasa limeamua kufanya maonyesho ya kiingilio cha fedha kila mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kupata pesa za kujikimu.
Uchaguzi mdogo katika jimbo hilo lililoachwa wazi na Rostam Aziz (CCM), aliyejiuzulu unatarajiwa kufanyika Oktoba 2 ambapo vyama vinane vya siasa vinashiriki
SOURCE:TANZANIA DAIMA

RAIS APOKEA TUZO MBILI KWA MCHANGO WAKE MKUBWA KATIKA AFYA YA MAMA NA MTOTO

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: 


Picture
Rais Kikwete akipewa tuzo na Waziri Mkuu wa Antigua and Barbuda, Winston Baldwin Spencer kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya afya, teknolojia na maendeleo kwenye hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na taasisi ya South-South katika hoteli ya Waldorf Astoria jijini New York, Jumatatu, 19.09.2011, usiku.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana (21 Septemba, 2011) amepokea Tuzo Mbili Maalum kwa mchango wake mkubwa katika Afya ya Mama Mjamzito na Watoto kwa ujumla kutoka taasisi mbili tofauti mjini New York.
Tuzo ya kwanza imetolewa na Taasisi ya Kijamii ya Umoja wa Mataifa (UN Foundation) na kukabidhiwa kwa Rais na Makamu wa Rais wake anayeshughulikia sera ya Umma Bw. Peter Yeo.

Rais amepokea Tuzo ya pili katika makao makuu ya Soko la Hisa la Marekani (National Association of Securities Dealers Automated Quotations) kwa kifupi NASDAQ ambalo ni soko la pili kwa ukubwa duniani baada ya lile la New York.  Rais amekabidhiwa tuzo hiyo na Makamu wa Rais wa NASDAQ Bw. David Wicks.

 Mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Rais amepewa heshima maalum ya kugonga kengele kuashiria mwisho wa biashara kwa siku hiyo.

Akipokea tuzo hizo mbili maalum, Rais ameelezea changamoto zinazoikabili sekta ya Afya nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla na kuzishukuru nchi na taasisi mbalimbali ambazo zinaunga mkono juhudi za kupunguza matatizo ya afya ya mama mjamzito.

Si sahihi kwa mama mjamzito kufariki wakati anampa uhai binadamu mwingine, uzazi unatakiwa kuwa shughuli ya furaha na sio huzuni na ndiyo maana tumetoa kipaumbele kwenye afya ya mama mjamzito kwenye ajenda yetu ya Afya” Rais amesema.

Rais amewaeleza wageni waalikwa ambao katika hadhara zote mbili wametoka katika nchi na taasisi mbalimbali kuwa kati ya vitu ambavyo serikali ya Awamu ya Nne imeamua kutoa kipaumbele katika kuongeza huduma za afya ya uzazi kwa kujenga zahanati na kuzipandisha daraja zilizokuwepo.

Serikali pia inaajiri wakunga na wataalamu zaidi wa Afya na kuongeza mafunzo katika sekta hiyo.

Juhudi zingine ni pamoja na kutoa huduma za Mpango wa Uzazi bure na kutoa vifaa vya kujifungulia kwa akina mama wanaohudhuria kliniki.

Vifaa hivi ni maalum kwa ajili ya kuwasaidia akina mama wakati wa kujifungua, na tuna amini kuwa kwa kufanya hivi wanawake wengi zaidi watahudhuria kliniki na kuwapa motisha wa kujifungulia katika taasisi zetu za afya”. Rais ameeleza.

Kutokana na juhudi hizo takwimu zinaonyesha kupungua kwa vifo vya akina mama wajawazito na  wakati wa kujifungua  kutoka 8,000 kwa mwaka 2005 hadi 6,000 mwaka jana.

Upungufu wa vifo 2,000 ni hatua nzuri katika muda mfupi lakini bado hairidhishi sana, tunaweza kupunguza zaidi na hilo ndiyo lengo letu kwani hatutaki kuona mwanamke yeyote anakufa kutokana na ujauzito au wakati wa kujifungua”. Rais amesema.

Mbali na shughuli hizo, Rais amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Slovenia Dr. Danilo Turk, Makamu Waziri Mkuu wa Luxembourg Bw. Jean Asselborn na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki Moon na Waziri wa Maendeleo wa Uingereza Bw. Andrew Mitchell.

Leo tarehe 22 Septemba, 2011, Rais anatarajiwa kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
MWISHO.

Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
New York.
Marekani.
22 Septemba, 201

HAWA NI MAKAMANDA

HARAKATI ZA IGUNGA

Walokole wachoma moto QURAN-MWANZA

Ni dhahiri vyombo hivi vya kiimani vimeanza kuyasahau majukumu yake na kutumiwa kufikisha sauti za wanasiasa nyuma ya migongo ya Imani na kutoa matamko katika mambo ambayo hakuna msingi wowote wa kiimani.

Ukweli hakuna dhambi inayoshinda nyingine, lakini kama ni uharaka na umuhimu wa kushughulikia mambo lipi la haraka zaidi kwa kuvuliwa kilemba DC na utovu wa maadili kwa baadhi ya waumini ambao wamerejea rasmi katika maasi baada ya TOBA ya RAMADHAN na hatujasikia Tamko.

Sasa wakati mnaendelea kupamba siasa za Igunga kwa ujira mdogo, usiku wa kuamkia leo waumini wa Dini ya walokole huko Mwanza wamechoma moto kitabu kitakatifu cha QURAN kwa madai ya kutakasa nyumba ya mmoja wa waumini wa dini ya kiislam aliyefanyiwa maombi maalum kumtanzua na kadhia ya maumivu ya miguu yanayomsumbua kwa muda mrefu sasa.

Mama huyo kutoka familia ya Bwana Adam Issa huko lumala Mwanza anadaiwa kufanyiwa maombi hayo hapo jana huku shemeji yake akiwa katika dimba la CCM kirumba kushuhudia mechi ya ligi kati ya Simba na Toto.


Kadhia hii inaelezwa kuleta tafrani kubwa katika hisia za waumini wa dini ya Kiisalm katika Kitongoji cha Lumala na kwamba hatua zaidi zitatangazwa baadaye.

BAKWATA na BASUTA sijasikia mkitoa tamko kuhusu hili licha ya kufuatilia Radio Imani asubuhi yote ya leo baada ya kupokea ujumbe huu kutoka mwanza kwa Shuhuda wa Tukio hili (Ninayemuamini na chanzo changu kwa habari zote za MZA)

My TAKE: Acheni siasa na majukwaa ya siasa yafanye kazi yake ''msichanganye Maandiko na siasa, ni kama Mafuta na Maji ''(MUNISHI)

Mazinde Juu-Lushoto

Wednesday, September 21, 2011

CCM haistahili kuendelea kuongoza

M. M. Mwanakijiji

WAKATI Baba wa Taifa amesema maneno yale “Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM”, sikuwa nimeyaelewa vizuri.
Sasa hivi maneno hayo hata hivyo yanapiga kelele katika mawazo yangu na kuacha mwangwi urindimao katika fikra zangu kila kukicha. Kama tunataka kweli kwenda na kufika kwenye ile nchi ya ahadi mambo kadhaa yanahitaji kutokea yakikihusu Chama cha Mapinduzi.
La kwanza ni kuwa CCM lazima ishindwe katika uchaguzi mkuu ujao na kwa kuanzia lazima ishindwe Igunga. Chama chochote tawala kinapokaa madarakani kwa muda mrefu kinajenga tabia mbili za hatari; moja ni tabia ya kuzoea na ya pili tabia ya ufisadi. Kwenye tabia ya kuzoea chama tawala kitakuja na kila aina ya mipango mizuri kwenye vitabu na kwenye makaratasi; vitazindua miradi ya kuvutia na kuanzisha kila aina ya kampeni. Matokeo yake chama hicho kinabakia kuwa ni chama cha “uzinduzi”.
Mara wamezindua barabara, mara wamefungua jengo fulani, mara wamezindua mradi wa visima vya maji n.k Wao sifa yao kubwa iko katika kuzindua vitu na kupiga picha za uzinduzi na kutamba kuwa mradi waliofungua wa wananchi umegharimu kiasi fulani. Na wananchi ambao wamezoea mambo ya kuzindua hujikuta wakisherehekea uzinduzi wa vitu visivyokoma. Hivyo chama kinakuwa na mazoea ya kuanzisha mambo tu. Sasa kuzindua peke yake hakutoshi lazima kuwa na ufuatiliaji endelevu wa yale yaliyozinduliwa.
Leo hii akipita mtu kufanya tathmini ya miradi mbalimbali ambayo imefunguliwa na serikali (ukiondoa ile ya wafadhili ambayo mara nyingi ina ufuatiliaji wa karibu) utashangaa ji kwa kiasi gani miradi ile imetunzwa kwa kiwango kinachostahili. Hebu mtu atembelee shule tulizozifungua miaka mitatu iliyopita kwa mbwembwe hadi kiongozi mmoja kututambia Bungeni kuwa tunapaa. Je, hizo shule leo zinaonekanaje? Je, bado zina mabati yote, milango na madirisha?
Sasa hiyo ni tabia ya mazoea. Yaani chama tawala kinakuwa na mazoea ya kuanzisha mambo bila ya kuyafuatilia ili kuyamaliza au kuhakikisha yanadumu kwa kiwango kinachostahili. Kwa hiyo kinakuwa chama cha mazoea ya mambo yale yale. Ndiyo maana leo hii maneno ya “kasi mpya, ari mpya, na nguvu mpya” huyasikii tena kwa sababu Chama tawala hakiwezi kuwa na “ari mpya, nguvu mpya, na kasi mpya” kikiwa na tabia ya mazoea!
Tabia ya pili ambayo inatokana na chama kuwa madarakani kwa muda mrefu ni tabia ya ufisadi. Tabia hii ya pili inatokana na hiyo ya kwanza (ya mazoea). Watumishi waliodumu muda mrefu katika chama tawala wanakuwa na mazoea ya kufanya mambo yale yale kwa mtindo ule ule na ni vigumu sana kwa wao kubadilika. Mazoea haya yanaanza kujenga tabia ya kuanza kutumia madaraka, vyeo, na nafasi mbalimbali kujinufaisha wao wenyewe huku wakiendelea kuzindua miradi mbalimbali kana kwamba wanafanya kitu fulani cha kushangilia. Sasa haina maana kuwa hawafanyi kitu ila kile wanachokifanya na kukitangaza kuwa wanafanya ni kiduchu kweli kulinganisha na kile ambacho wangeweza kufanya au wanapaswa kufanya.
Sasa huu ufisadi unatokea taratibu kwa sababu kwa vile wamezoeana na wanajuana inakuwa vigumu kweli kwa wao wenyewe kuwajibishana kiasi kinachostahili. Matokeo yake utakuta kuna tabaka la aina fulani la ufisadi unaokubalika katika jamii.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe akiandika kwenye mtandao maarufu duniani wa Watanzania wa jamiiforums.com ameelezea kisa cha mzee mmoja ambaye alikuwa anatafuta haki yake kutoka kwenye idara moja nyeti ya serikali (TRA). Mzee huyo baada ya kuhangaika kwa muda mrefu alijikuta kila anakokwenda ili aweze kutatuliwa tatizo lake alihitaji kutoa ahadi kuwa mambo yakimuendea basi “awakatie” watumishi waliomsaidia kitu kidogo.
Mzee huyo hakuwa tayari kufanya hivyo. Alipopata nafasi ya kumuelezea Kabwe juu ya suala lake na Zitto alipoamua kuandika barua kwa Waziri Mkuu, Mzee yule kwa mujibu wa Mhe. Zitto akainama na kuniambia, “ Mheshimiwa Zitto (ninamquote hapa maana sipendi kuitwa mheshimiwa) kama ukifanikiwa kunisaidia suala hili, nitakujengea nyumba nzuri Kigoma'”
Sasa Zitto anaelezea mwitikio wake “Kalamu ilianguka kwa kutetemeka kwa hasira; Mratibu wa ofisi yetu alikuwa ananiangalia na akitarajia kuachana na mzee huyu. Nilimtazama mzee huyu na kumwambia 'Baba, hii ni haki yako huna haja kuinunua. Mimi pia hii ni kazi yangu, ninalipwa kuifanya. Sitaki nyumba yako. Sitaki chochote kutoka kwako”
Sasa mtu anaweza kuguswa na mwitikio wa Zitto lakini ukiangalia vizuri mwitiko wake ulipaswa kuwa hivyo. Lakini kubwa zaidi (tukiamini simulizi la Zitto) ni ujasiri wa Mzee huyo mwenye shida pasipo woga, haya wala kufikiria anachosema kutoa “hongo” namna hiyo. Ukiangalia utaona kuwa katika sehemu nyingi za jamii yetu tumezoea mno vitendo vya ufisadi kiasi kwamba wakati mwingine hata hatufikirii mara mbili. Hii inatokeana na kujengeka katika jamii yetu kwa utamaduni wa kifisadi ambao msingi wake ni utawala wa muda mrefu wa chama kimoja.
Sasa, ili mambo yaweze kugeuka ni lazima CCM ishindwe uchaguzi wa Igunga ili hatimaye tuweze kuanza upya kujenga Taifa letu jinsi ile ambavyo tunataka.
Lakini jambo jingine ambalo linatokana na hilo la CCM kupoteza uchaguzi ni kuwa aidha CCM kama ilivyo ishindwe kwenye uchaguzi huo au ilazimishwe kushindwa toka ndani yake yenyewe.
Kuilazimisha kutoka nje ni kwa kutokea chama kingine ambacho siyo tu kina sera nzuri lakini wananchi wanaweza kuamini kuwa kinaweza kweli kuchukua madaraka ya nchi na kesho wake wananchi wakaenda zao sokoni, kazini, na shuleni kama kawaida pasipo kukaa na kusikiliza redioni nini kimetokea.
Njia hii ya kuwa na chama mbadala ni bora zaidi na ya kuaminika zaidi kwani italeta nchini siasa mpya ambapo wananchi wanaweza kubadilisha vyama hivi pasipo kuwa na matatizo yoyote au kufikiria mara mbili kwani wanajua vyote viwili vinaweza kuunda serikali na kushikilia nchi.
Mfano mzuri ni uchaguzi wa Marekani ambapo chama cha Repablikani kimepoteza nafasi ya Urais, na mabaraza yake mawili ya Uwakilishi kufuatia ushindi wa Seneta Barack Obama.
Kwa sababu Wamarekani hawana hofu nani anayechukua madaraka kila baada ya miaka minne kwani wanajua akiwazingua wanamtimua miaka minne ijayo! Katika Tanzania bado hili ni gumu kama tulivyoshuhudia kwa majirani zetu Kenya na Zimbabwe. Hivyo, hili la kuwa na chama mbadala ni muhimu sana kama kweli tunataka kujenga utawala wa kidemokrasia, huu utitiri wa vyama tulionao unapoteza muda, unatawala vipaji, na kamwe hautaleta chama mbadala. Lakini kuombea hilo kwa sasa ni sawa na kusubiri mvua za masika jangwani!
Ambalo linapaswa kutokea ni kile ambacho kinatokea Afrika ya Kusini sasa hivi. Chama cha Mapinduzi ni lazima kimeguke kama kweli kinataka kurudi kwenye misingi yake na kushiriki upya katika ujenzi wa taifa jipya la Kitanzania kwani kilivyo sasa kinakwenda kwa kuvutana kamba.
Ili kiweze kumeguka kweli kinahitaji ndani yake watu watakaogongana kimawazo na kimtazamo. Ni lazima utokee mgongano wa kifikra, kiuongozi, na kimwelekeo ili CCM iweze kuwa na kambi kubwa mbili ambazo haziwezi kukaa pamoja na hazipaswi kukaa pamoja. Kule Afrika ya Kusini baada ya kambi ya Zuma kujipanga vizuri na hatimaye kumnyima Mbeki uenyekiti wa ANC na baadaye kuhakikisha kuwa Mbeki anakuwa dhaifu ndani ya Chama hatimaye waliweza kusababisha Mbeki kuachia ngazi mapema kabla ya muda wake.
Kama kina Zuma walitarajia Mbeki angeondoka kimya kimya walifanya makosa na matokeo yake mashabiki wa Mbeki wameamua kujimega kutoka ANC na kuunda chama kingine cha kisiasa.
Sijui ni kwa kiasi gani chama hicho kitakuwa na nguvu katika siasa za Afrika Kusini kwani yawezekana kukawa na mambo ya kikabila au majimbo ndani yake lakini kwa vyovyote vile kunailazimisha ANC aidha kubadilika au kujikuta inabadilishwa.
Hilo ndilo linalohitajika kutoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi. Hata hivyo haliwezi kutokea hadi pale baadhi ya “vigogo” wa chama hicho hasa wakongwe au wale ambao wamejikuta wakiwekwa pembeni kutokana na misimamo yao watakapoamua kujitoa ndani ya chama hicho na kuanzisha chama kingine. Hili litawezekana tu pale ambapo wakongwe walioko CCM watakapotambua mioyoni mwao kuwa CCM siyo mama yao. Pale watakapotambua kuwa wanaweza wasife wana CCM lakini watakufa wakiwa ni Watanzania!
Sasa hivi heshima kubwa ambayo baadhi yao wanayo (kama alivyosema Mzee Kawawa miaka ile) ni kuhakikisha kuwa wanakufa wakiwa wana CCM pia. Wengine kati yao wameapa kabisa kuwa liwalo na liwe wao ni “wana CCM mpaka kufa”. Nakumbuka wengine wetu tuliimba nyimbo za “naapa naahidi mbele ya Chama, Mapinduzi nitakulinda mpaka kufa”. Lakini ahadi hiyo ni ya uongo kwani utii na mapenzi yetu kama raia wa taifa letu hayawezi kamwe kuwa kwa mtu, idara, taasisi au chama cha kisiasa. Mapenzi na utii wetu wa kwanza na wajuu zaidi ukiondoa ule ulioko kwa muumba wetu ni kwa nchi yetu.
Wazo hili litakapoingia ndani ya viongozi wa CCM hasa wale ambao kweli wanaamini mabadiliko yanahitajika haitawachukua muda kuamua kujitoa ndani ya CCM na kuanza harakati za kuleta mabadiliko ya kweli.
Hili hata hivyo haliwezi kuwa jambo la mtu mmoja mmoja kama ilivyokuwa kwa Ndg. Mrema (mwenyekiti wa sasa wa TLP). Kujiondoa kwa mtu mmoja ndani ya CCM haitoshi inabidi kundi zima la wana CCM mahiri na mashuhuri liamue kujitoa ndani ya chama hicho kama ishara ya kuchoshwa na mambo yalivyo lakini pia kama alama ya kutaka kuanza upya.
Tatizo kubwa la mpango huo ni kuwa kuna dalilii kuwa wale watakaotoka yaweza kuwa ni wale ambao tayari wamekataliwa na wananchi na hawana ule “ujiko” wa kisiasa au mtaji wa kisiasa wa kuwaweza kufanya kuwa na nguvu nchini. Lakini endapo watakaotoka ni wale ambao wananchi wamewaona ni watetezi wao, wapiganaji wao, au kwa namna fulani wanasimamia maslahi ya Taifa basi CCM itakuwa kweli imepata mpasuko unaostahili.
Kumeguka huko kwa CCM kutasababisha mgongano wa kifikra katika taifa, mgongano ambao utachuja makapi na nafaka na kuchuja viongozi uchwara na wenye masihara kutoka katika viongozi walio bora. NI mgongano ambao mbegu zake tumekuta tukizipanda taratibu.
Hakuna kitu ambacho kinaitisha CCM na watawala wake kama wagombea huru. Wagombea huru wasiofungamana na chama chochote ni tishio kubwa kwa CCM kuliko upinzani uliopo sasa. Sababu kubwa ni kuwa wagombea huru hawafungwi na nidhamu ya chama fulani au woga kwa “mwenyekiti wa chama”. Wao wanafungwa na wapiga kura wao. Ni kwa sababu hiyo CCM imejitahidi sana kukwepa kuruhusu wagombea binafsi kwa sababu endapo watafanya hivyo watakuwa wameamua kutumia mafuta yao wenyewe kukaangwa.
Hata hivyo naamini kabisa ya kuwa ni kwa maslahi ya taifa wabunge wa CCM waiteke hoja ya wagombea binafsi na kuilazimisha kwa nguvu ya kisheria. Kama serikali yenyewe haitaki kuleta mswaada wa mabadiliko hayo ya sheria wakati umefika kwa mbunge mahiri wa CCM kuleta mswada binafsi wa kuleta mabadiliko hayo. Sababu kubwa ni kwamba, wakileta mabadiliko ya sheria hiyo ni wazi kuwa wabunge wengi waliopo sasa ndio watakuwa wa kwanza kufaidika nao hasa kama CCM itaendelea kutumia mfumo wake wa kura za maoni na maamuzi ya Kamati Kuu katika kutafuta wagombea wake.
Vinginevyo, bado ninaamini ya kuwa kumeguka kwa chama cha Mapinduzi ni muhimu kutokea ili hatimaye Taifa letu liweze kuanza upya safari ya maendeleo. Sababu kubwa ni kwamba CCM imetawala muda mrefu na haiwezi kubadilika au kujibadilisha.
CCM imeendelea kutawala kwa kawaida huku ukifanya mazingaombwe ya kuonesha inabadilika kumbe inabakia vile vile; na CCM hata kama ikipigiwa mbiu ya mgambo haiko tayari kujisafisha na kuleta mabadiliko ya kweli ya taifa kwa kadiri ya kwamba hali iliyopo inainufaisha yenyewe.
Ndiyo maana utaona kuwa mambo yanayohusu CCM wako tayari kuyadili kwa kina kuyachukulia hatua madhubuti lakini yanapokuja yale yenye umuhimu kwa Taifa inabidi hadi watu waandamane. Hebu fikiria suala la EPA peke yake hadi watu kufikishwa mahakamani lilichukua muda gani?
Na hapo hatujaanza kuangalia suala la Meremeta, Mwananchi Gold, Deep Green Finance, Kagoda, rada, malori, helikopta, majengo ya BoT n.k Kama jambo moja tu limechukua miaka miwili haya yote yakijakumalizwa kuna wengi wetu hapa tutakuwa tumeshaondoka katika ulimwengu huu na wajukuu zetu wakiandalia kuhangaika nayo! Kwa kadiri tunakubali na kushangilia mazingaombwe tunayoyaona ndivyo hivyo na wenyewe hawaoni haraka ya kufanya jambo lolote kwa sababu wamezoea jinsi ilivyo.
Lakini vyovyote vile ilivyo, kama kweli Tanzania inataka kupati nafasi ya kufanikiwa na kuanza kuelekea nchi ile tuitamaniyo, CCM kama ilivyo sasa haistahili kuendelea kuliongoza taifa letu baada ya 2010.
Aidha, wanyang’anywe urais (kama ilivyotokea Afrika Kusini, au wanyang’anywe Bunge (kama ilivyotokea Kenya), au wanyang’anywe vyote viwili (kama ilivyotokea Marekani). Kuwaachia waendelee walivyo sasa, ni kuwapa baraka ya kutudumaza.