Friday, September 23, 2011

MIKATABA INAVYOSAINIWA


Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe (mwenye furana ya njano kati )
akiwa na viongozi wa wadau mbali mbali wa Ludewa
baada ya kumaliza hafla fupi ya kusaini mkataba huo.






Nakumbuka mwaka huu katika kikao cha Bunge, ndani ya bunge au nje ya bunge, Mhesh. Deo F. Haule Mbunge wa Ludewa alipata kutamka kwamba Katibu wa Wizara ya madini David Jairo alikuwa kizuio cha kusaini mkataba wa mradi wa madini Ludewa.

Kwenye habari hiyo hapo chini:
Akizungumza na waandishi wa habari,
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya NDC Bwana Mzindakaya alisema, kuna watanzania wenzetu ambao wanafanya kila jitihada ili kuhakikisha mradi huo unakwama lakini yeye amesema hakuna mtu tena atakayediriki kuuzuia mradi huo usianze kwani huo ni mradi wa Taifa
Baada ya Jairo kuwekwa mahabusu ya nje, mradi wa Makaa ya mawe na chuma Ludewa umeenda chapuchapu na kusainiwa. Je Jairo alikuwa kizuio? Jairo ana mfumo dume wa kujali maendeleo ukanda aliotoka tu na kutojali maendeleo kitaifa?

Subira yavuta heri ama hayawi hayawi sasa yamekuwa ndivyo wanavyoweza kusema wakazi wa wilaya ya Ludewa mkoa wa Iringa ama mkoa mpya wa Njombe baada ya Ule mradi ambao ulionekana kuwa ni ndoto ya mchana, mradi wa makaa ya mawe wa Mchuchuma na Mradi wa Chuma wa Liganga utaanza muda wowote baada ya kusainiwa leo mchana.

Akithibitisha baada ya kushuhudia tukio hilo, Mbunge wa Ludewa Mhe. Deo Filikunjombe amesama leo LUDEWA IMEPATA UHURU. Miaka nenda rudi ilikuwa ni historian a maelezo mengi tu kuhusu Miradi hiyo miwili lakini leo Mkurugenzi wa bodi ya Wakurugenzi wa National Development Corporation NDC Bwana Chrisant Mzindakaya amesaini kwa niaba ya serikali na mwakilishi wa kampuni Liu Canglong alisaini kwa niaba ya kampuni ya Hongda Group ya China.

Mradi wa Liganga una chuma kiasi cha tani 1.2 bilioni na utaanza kuzalisha tani milioni tatu kwa mwaka na mradi wa mchuchuma utakuwa na uwezo wa kutoa tani milioni tatu za chuma kwa mwaka. Mradi wa Mchuchuma una kiasi cha tani 400 milioni za makaa yam awe ambayo yanaweza kuchimbwa kwa zaidi ya miaka 500. Kabla ya kuanza miradi hiyo, Mzindakaya alisema itachukua hadi miezi sita ili kuhakiki na kutathmini thamani halisi ya makaa ya mawe na itahitajika miezi hadi 36 kutathmini chuma ghafi huko Mchuchuma na Liganga.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi baada ya kusainiwa mkataba huo, Mbunge wa Ludewa Mhe. Deo Filikunjombe alisema, licha ya faida zitakazotokana na hisa za serikali ambazo kwa awamu ya kwanza zitakuwa 20%, kutakuwa na faida nyingine lukuki zikijumuisha, maendeleo ya viwanda vidogo vidogo, viwanda vya chuma, ujenzi wa miundo mbinu ya reli, barabara ya lami, mfumo wa kusafirishia umeme, bandari, viwanja vya ndege na makazi ya watu. Kuhusu mapato ya serikali Mhe. Filikunjombe alisema, kutakuwa na mapato ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 1.2 au shilingi za Kitanzania takribani trilioni 2 zitakazotokana mauzo ya mazao ya chuma na umeme kwa mwaka. Hivyo inatarajiw serikali itapata mapato mengi kupitia kodi mbalimbali.

Mradi utakuwa unaajiri wafanyakazi 8000 kila mwaka na mradi wa umeme utaanza kutoa umeme wa MGW 600 ambazo zitatengenezwa kwa namna ambayo itakuwa ni rahisi kuuongeza nguvu na kutengeneza MGW zitakazohitajika na Taifa.
Sherehe hizo zilihudhuriwa na Makamu wa Rais, Mhe. Ghalib Bilal ambaye alikuwa mgeni Rasmi pamoja na viongozi wengine wa chama, serikali, vyama vya siasa, wazee wawakilishi kutoka Ludewa, Mkuu wa wilaya ya Ludewa Mhe. Na viongozi wengine kutoka wilaya ya Ludewa. Kulikuwa vile vile na wawakilishi kutoka kampuni ya Hongdan Group waliokuja na ndege mbili kutoka China pamoja na wadau wengine wa miradi hiyo ya Maendeleo.

Habari zaidi kuhusu namna Taifa litakavyofaidika na miradi hiyo zitatolewa baada ya muda si mrefu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya NDC Bwana Mzindakaya alisema, kuna watanzania wenzetu ambao wanafanya kila jitihada ili kuhakikisha mradi huo unakwama lakini yeye amesema hakuna mtu tena atakayediriki kuuzuia mradi huo usianze kwani huo ni mradi wa Taifa.

No comments:

Post a Comment