Tuesday, September 06, 2011
| Na Joyce Kasiki, Dodoma
MWANAFUNZI mmoja wa darasa la saba wa shule ya msingi Kibakwe wilayani Mpwapwa kesho Jumatano atashindwa kufanya mtihani wa darasa la saba kutokana na kupewa mimba na Mwalimu Mkuu wake wa shule ya hiyo Anord Ng’undu (35).
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Robarti Kitimbo alifafanua kuwa Mwalimu huyo anashikiliwa na jeshi la polisi katika kituo cha polisi cha Mpwapwa.
“Taarifa za za mwanafunzi huyu mwenye umri wa miaka 13 mimi nilizipata kutoka kwa watendaji wangu wa juu ambapo alikuwa anafanya jaribio la kuitoa mimba hiyo kwa kutumia madawa ya kienyeji nyumbani kwao kijiji cha Ikongola Kibakwe”alisema
Alisema kuwa kutokana na jaribio hilo hatua zaidi za kisheria zilichukuliwa kwa kumuhoji mawanafunzi huyo ambapo alimtaja mwalimu huyo kuwa ndiye muhusika mimba hiyo.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa mwanafunzi huyo hivi sasa amelazwa katika hospitali ya Benjamini Mkapa kwa ajili ya uchunguzi na kupatiwa matibabu.
Kwa upande wake mganga mkuu wa Hospitali hiyo ya Benjamini Mkapa Dkt Ibrahim Katunda alikiri kumpokea mwanafunzi huyo ambaye amelazwa katika wodi namba nane.
Alifafanua kuwa mwanafunzi huyo amepokelewa hospitalini hapo na kwamba anafanyiwa uchunguzi.
Naye Mkuu wa Wilaya hiyo Darry Rwegasira alikiri kupokea taarifa hizo za mwalimu huyo kushikiliwa na jeshi la polisi.
Alifafanua kuwa suala hilo ni la kisheria hivyo amewaachia jeshi la polisi pamoja na madaktari kwa lengo la kufanya uchunguzi wao ili kubaini ukweli wa suala hilo la mimba.
No comments:
Post a Comment